
Reus alizaliwa katika Jiji la Dortmund, Mei 31, 1989 na alianza kucheza soka katika timu ya vijana ya Post SV Dortmund mwaka 1994.
Reus alizaliwa katika Jiji la Dortmund, Mei 31, 1989 na alianza kucheza soka katika timu ya vijana ya Post SV Dortmund mwaka 1994 lakini miaka miwili baadaye mwaka 1996 alijiunga na timu ya vijana ya Borussia Dortmund.
DORTMUND, UJERUMAN
KAMA kuna mchezaji wa Borussia Dortmund anayezitoa udenda timu nyingi za England kwa sasa, achilia mbali, Ilkay Gundogan, basi Marco Reus anaongoza.
Si Manchester United, Arsenal, Manchester City wala Chelsea ambayo haijahusishwa kumchukua fundi huyu wa timu ya Taifa ya Ujerumani. Ni nani huyu Marco Reus?
Ana damu ya Dortmund
Reus alizaliwa katika Jiji la Dortmund, Mei 31, 1989 na alianza kucheza soka katika timu ya vijana ya Post SV Dortmund mwaka 1994 lakini miaka miwili baadaye mwaka 1996 alijiunga na timu ya vijana ya Borussia Dortmund.
Mwaka 2006 alijiunga na timu ya Rot Weiss Ahlen kuchezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 19. Baadaye akafanikiwa kupenya mpaka timu ya wakubwa. Alifunga mabao mawili katika mechi 14.
Msimu wa 2008–09, akiwa na umri wa miaka 19 alijitambulisha kwa kiasi kikubwa katika soka akicheza mechi 27 na kufunga mabao manne.
Asaini Monchengladbach, akoshwa na Rosicky
Mei 25, 2009, alisaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Borussia Monchengladbach inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani. Agosti 28, 2009, Reus alifunga bao lake la kwanza Bundesliga dhidi ya Mainz 05 akikimbia umbali wa mita 50 na kumfunga kipa kiurahisi. Tangu hapo alikuwa mfungaji mahiri wa kikosi cha Kocha Lucien Favre.
Msimu wa 2011–12, Reus aliuanza akiwa fomu kwa kufunga mabao saba katika mechi 12 tu. Akiwa hapo, mwenyewe alikaririwa akisema kwamba shujaa wake alikuwa kiungo wa sasa wa Arsenal, Tomas Rosicky ambaye aliwahi kuichezea Borussia Dortmund kwa miaka sita kabla ya kuhamia Arsenal mwaka 2006.
Atua Borussia Dortmund
Januari 4, 2012, Reus alisaini klabu yake ya zamani, Borussia Dortmund ambayo aliichezea timu yao ya vijana. Uhamisho huo uligharimu kiasi cha Euro 17 milioni na alisaini mkataba wa miaka mitano.
Hata hivyo, Reus aliendelea kuichezea Monchengladbach na kujiunga rasmi na Dortmund Julai Mosi, 2012. Alifunga bao katika mechi yake ya kwanza ya Dortmund dhidi ya Werder Bremen ambayo walishinda 2-1 Agosti 24, 2012. Akafunga mawili dhidi ya timu yake ya zamani, Borussia Monchengladbach katika ushindi wa 5-0, Septemba 29.
Alifunga bao lake la kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City katika sare ya 1-1 ugenini, akafunga tena katika sare ya 2-2 dhidi ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu akipiga shuti kali akipokea pasi ya Robert Lewandowski. Akafunga jingine katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Ajax, hiyo ilikuwa Novemba 2012.
Februari 16, 2013 alifunga mabao matatu yote ya ushindi dhidi ya Eintracht Frankfurt na Mei 11, akafunga mabao mawili ya kusawazisha yakiiokoa Dortmund mbele ya Wolfsburg.
Msimu huu, Reus ameendelea kuwa moto na aliuanza kwa kufunga bao la kuongoza katika ushindi wa mabao 4-2 mechi ya ufunguzi wa msimu wa soka Ujerumani dhidi ya Bayern Munich Julai 27, 2013.
Akafunga bao la penalti dhidi ya Eintracht Braunschweig katika ushindi wa 2–1. Akafunga mawili dhidi ya Freiburg, moja likiwa la penalti. Mwenyewe alikaririwa akisema kwamba atapiga penalti zote za Dortmund msimu huu isipokuwa zile ambazo atasababisha mwenyewe.
Na kweli, wakati Reus aliposababisha penalti dhidi ya 1860 Munich, winga mpya wa Dortmund, Pierre Aubameyang ndiye alipiga penalti hiyo. Novemba Mosi mwaka huu akafunga bao moja katika ushindi wa 6-1 dhidi ya Stuttgart.
Atesa na kizazi kipya Ujerumani
Reus ameichezea Ujerumani katika ngazi zote, lakini aliitwa kuchezea timu ya wakubwa mechi ya kwanza Mei 14, 2010, dhidi ya Malta. Hakuweza kucheza kutokana na kuumia. Alicheza mechi ya kwanza dhidi ya Uturuki Oktoba 7, 2011. Alifunga bao lake la kwanza katika kichapo cha 5-3 kutoka kwa Uswisi Mei 26, 2012. Juni 22, 2012 akafunga bao katika pambano la robo fainali Euro 2012 dhidi ya Ugiriki.
Aongoza kwa kufunga mabao Ujerumani
Katika kikosi cha sasa cha Ujerumani chini ya Kocha Joachim Low, Reus ndiye amefunga mabao mengi katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2014. Amefunga mabao matano katika mechi tano.
0 comments:
Post a Comment