
Cristiano Ronaldo, licha ya jina kubwa katika ulimwengu wa soka, anaweza akapunguza utamu wa fainali za Kombe la Dunia mwakani kama timu yake ya Ureno itashindwa kulinda bao alilofunga Ijumaa katika mechi ya kwanza ya mtoano dhidi ya Sweden walipokuwa nyumbani Ureno.
SHARE THIS STORY
LEO Jumanne usiku kabla haujalala, staa mmoja duniani atakosa rasmi kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil na mwingine atakata tiketi na kufunga begi kwenda Brazil katika fainali hizo kubwa duniani.
Cristiano Ronaldo, licha ya jina kubwa katika ulimwengu wa soka, anaweza akapunguza utamu wa fainali za Kombe la Dunia mwakani kama timu yake ya Ureno itashindwa kulinda bao alilofunga Ijumaa katika mechi ya kwanza ya mtoano dhidi ya Sweden walipokuwa nyumbani Ureno.
Lakini hata Zlatan Ibrahimovic ambaye jina lake linatamba katika soka kwa sasa, huenda asifunge begi lake kwenda Brazil mwakani kama timu yake Sweden itafungwa au kuambulia sare yoyote katika ardhi ya nyumbani katika pambano hilo la marudiano.
Mpaka sasa katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia la mwakani, Ibrahimovic, maarufu kwa jina la Ibracadabra kutokana na maajabu yake uwanjani, anaongoza kwa kuifungia Sweden mabao akiwa amefunga mara sita wakati anayeshika nafasi ya pili, Johan Elmander amefunga matatu.
Kwa upande wa Ronaldo, licha ya kutawala katika soka la Hispania, lakini anakamata nafasi ya pili katika ufungaji wa mabao akiwa na mabao manne sawa na beki, Bruno Alves, huku mshambuliaji, Helder Postiga akiongoza kwa mabao sita. Wakati vita ikionekana kuwa ya binafsi zaidi kati ya Ronaldo na Ibra, vita nyingine katika pambano hilo itakuwa katika eneo la kiungo ambapo kwa Ureno huwa linadhibitiwa na kiungo wa Monaco, Joao Moutinho, ambaye alikuwa mchezaji bora wa pambano la Ijumaa nyumbani Ureno.
Achilia Moutinho, Ureno inajivunia winga wa Manchester United, Luis Nani na kiungo wa Fenerbahce, Raul Meireles, lakini itajikuta katika wakati mgumu mbele ya viungo wa Sweden, Anders Svensson, Alexander Kacaniklic na Pontus Wernbloom.
Kuweza kutawala pambano hilo, Ronaldo analazimika kufanya kazi ngumu dhidi ya beki, Bruno Alves, wakati Zlatan atakutana na wakati mgumu kwa mara nyingine tena kumpita beki mkorofi wa Real Madrid, Pepe ambaye alimkaba vema katika pambano la Ijumaa iliyopita katika ardhi ya Ureno.
Ureno ilishinda 1-0 Ijumaa.
0 comments:
Post a Comment