
Kiraka wa Taifa Stars, Shomari Kapombe akiwaongoza wenzake kupasha jana Jumatatu jioni kwenye Uwanja wa Taifa. Mchezaji huyo anayechezea AS Cannes ya Ufaransa ameungana na kikosi hicho Dar es Salaam.
IN SUMMARY
- Samatta na Ulimwengu wote wanaichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameungana na wenzao kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa). Mchezaji mwingine wa nje aliyemo Stars ni kiungo wa Mwinyi Kazimoto wa Al Markhiya ya Qatar na Shomari Kapombe wa AS Cannes ya Ufaransa.
MASTRAIKA wa Tanzania wanaocheza nje, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta, wameahidi soka la aina yake kwenye mechi ya kirafiki baina ya Taifa Stars na Zimbabwe leo Jumanne jioni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Zimbabwe ambayo itashiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) mwakani, iliwasili jana Jumatatu ikiwa pamoja na wakali wake wawili wanaocheza Ligi Kuu Afrika Kusini ambao ni Tapuwa Kapini (kipa) na Carlington Nyadombo (beki) wote wa Amazulu FC.
Samatta na Ulimwengu wote wanaichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameungana na wenzao kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa). Mchezaji mwingine wa nje aliyemo Stars ni kiungo wa Mwinyi Kazimoto wa Al Markhiya ya Qatar na Shomari Kapombe wa AS Cannes ya Ufaransa.
Ulimwengu alisema: “Timu ipo vizuri na tumefanya maandalizi ya kutosha ambayo yananipa matumaini kuwa tutashinda mechi, Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kuona vijana wao tukijitolea. Pia nimefurahi kuona idadi kubwa ya vijana kikosini.
“Ni jambo zuri kwa sababu vijana ndiyo kila kitu, kama watakuwa na msingi mzuri kwa sasa, baadaye tutakuwa na timu nzuri itakayofanya vizuri na kutimiza ndoto za Watanzania.
“Unajua kitu ambacho tunakosea sisi Watanzania ni kutokuwa na subira, tunataka mafanikio ya haraka wakati si sahihi, timu kubwa zenye mafanikio zilianzia huku kwa vijana, wakaweka msingi mzuri ndiyo maana zinafanya vizuri sasa.”
Naye Samatta alisema: “Tuna kila sababu ya kushinda mechi hii, sote tutaingia kwa ajili ya kutafuta ushindi tu ili Watanzania wafurahi.”
Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Kim Poulsen, alisema: “Ni mechi ya kujipima nguvu, lakini ni muhimu na tunataka kushinda.”
0 comments:
Post a Comment