
Anajulikana ulimwenguni kote kama “Rais Masikini Kupita Wote Duniani” (World’s Poorest President). Ni Rais Jose Mujica wa Uruguay nchi ndogo tu iliyopo Amerika ya Kusini na maarufu kwa uchezaji wake wa mpira wa miguu(soka).
Hivi karibuni Rais Jose Mujica ameushangaza ulimwenguni kwa kuifanya Uruguay kuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu kwa ujumla kabisa matumizi ya bangi. Sheria tayari imepita katika Bunge na inatarajiwa kupita katika Seneti baadae mwaka huu na kuifanya Uruguay kuwa nchi ya kwanza duniani kutoa leseni za biashara ya Bangi na kusimamia sheria na taratibu za uzalishaji na usambazaji na mauzo ya bangi kwa watumiaji watu wazima.
Rais Mujica ambaye pia anajulikana kama Pepe Mujica, ana umri wa miaka 78. Mpaka leo hii amekataa kuhamia katika jumba la kawaida la kifahari la Rais na badala yake amebakia katika nyumba yake ndogo tu ya kawaida ambapo anaishi yeye na mke wake ambaye ni Seneta.
Anachangia asilimia 90 ya mshahara wake kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa nyumba kwa wanawake wasio na wanaume.
Mtizame katika mahojiano haya hapa chini na kipindi cha Talk to Al-Jazeera cha kituo cha televisheni cha Al-Jazeera.
0 comments:
Post a Comment