Wiki chache zijazo kundi linaloundwa na vijana wawili mapacha kutoka nchini Nigeria, Paul andPeter Okoye la P-Square, litatua jijini Dar-es-salaam maalumu kabisa kwa ajili ya kupiga show moja tu! Show hiyo, kwa mujibu wa ahadi za waandaji na wadhamini (East Africa Television,East Africa Radio na Vodacom Tanzania,itakuwa ya aina yake, yenye kuleta mapinduzi na ambayo haijawahi kutokea. Kwa maana hiyo, show ya P-Square ambayo imepewa jina la P-Square Live in Dar, itaweka historia mpya. Bila shaka hili ni jambo la kusubiriwa.
Kwa mujibu wa waandaji wa show ya P-Square, show hii yote itapigwa Live kwa maana ya kwamba bendi itakuwa ikinyuka kila kitu Live na sio muziki wa kuimbiwa playback kwenye CD.P-Square watatua na bendi ya watu 13 ili kukamilisha zoezi hilo na kutimiza ahadi hiyo.
Ujio wa P-Square nchini unakuja katika kipindi ambacho binafsi naamini ni kipindi ambacho muziki wa Bongo hususani huu wa kizazi kipya unahitaji mabadiliko fulani ili nao angalau uweze kutanuka zaidi nje kuvuka ukanda wa Afrika Mashariki. Naamini wakati sasa umefika kwa wasanii wa Tanzania nao kuonekana kwenye majukwaa ya kimataifa kwa maana ya kimataifa kama ambavyo hapo zamani wasanii na wanamuziki kama vile Hukwe Zawose, The Kilimanjaro Band, Dr.Remmy Ongala na wengine walifanikiwa kufanya. Ndio maana naamini kwamba yapo mambo kadhaa ambayo wasanii wetu wanaweza kujifunza kutoka kwa P-Square.
- Kufanya maonyesho “Live”- Miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakichangia katika kudumaza muziki wa kizazi kipya Tanzania imekuwa ni tabia ya kuimbia juu ya CD yaani CD Playback. Tabia hii imekomaa kiasi kwamba imeonekana kama kukubalika. Sio sahihi. P-Square wanakuja na bendi ya watu 13.Watapiga muziki wa moja kwa moja. Hili wasanii wetu wanaweza kuliiga. Ni jambo zuri na la kimaendeleo endapo wasanii wetu wana nia ya dhati ya kupambana katika majukwaa ya kimataifa.
- Kujithamini kama wasanii- Ukweli ni kwamba P-Square ni wa ghali. Ukisikia bei ya kuwaleta wasanii hao Bongo utaelewa kwamba Yes jamaa wanajithamini. Lakini pengine wanajithamini na kujiwekea kiwango cha juu cha pesa kwa sababu wanajua fika kwamba wakipanda jukwaani wanafanya kazi kweli kweli ikiwemo hiyo ya kuimba “Live”.Maana tuseme ukweli,kama unakuja kuimba playback halafu uniambie unataka milioni 10 kwa show,dah…huoni kama ni wizi huo?
- Kujitangaza kimataifa. Wasanii wetu wanaridhika sana na mafanikio kiduchu tu. Akiona akienda Morogoro Uwanja wa Jamhuri unafurika na shangwe basi anaona amemaliza. Ingekuwaje P=Square wangeishia kwenye viunga vya kwao Nigeria?
- Kuwa na malengo ya uhakika- Nimesoma mahali kwamba P-Square tangu wanaanza walikuwa na malengo makubwa. Walitambua kwamba pamoja na kwamba wangeweza kuwa matajiri hapo hapo kwao Nigeria(Nigeria ina watu milioni 170. Kama nusu au hata robo tu ya watu wakinunua CD halali,wameula). Wao walitizama mbele zaidi
0 comments:
Post a Comment