Taarifa za kipa nyota, Juma Kaseja kutua Yanga zimewachanganya watu wengi.

Ingawa zimekuwa hazina uhakika, lakini Salehjembe imepata taarifa za uhakika kwamba mchana huu ndiyo amemalizana na Yanga.

Lakini bado watu wamekuwa wakihaha kutaka kujua kuhusiana na suala hilo.

Mmoja wa viongozi wa Yanga alisema; “Sitaki kulizungumzia kwa sasa, kama kuna walioandika sawa, lakini kumalizana kwetu na Juma ni leo (Alhamisi).

“Tulimpa mkataba, anao yeye, hivyo tutakutana na kumalizana leo na tumegawanya makundi mawili, moja litakuwa uwanjani katika mechi dhidi ya Oljoro na lingine katika ishu hiyo ya Kaseja.”

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About