
Mweusi Joh Makini yeye hana tatizo kabisa na jina hilo na anaamini linaweza kutumika vizuri kuwakilisha muziki mzuri wa kizazi kipya wa Tanzania, lakini anachoona hakiendi sawa ni pale ambapo kila anaejaribu kuimba anaingia kwenye hili bus la Bongo Fleva.
Joh Makini alifunguka akiwa ndani ya ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times fm, walipoweka mjadala huu mezani akiwa na Saleh Jabir aka Kuvichaka, Dj Ommy na mkali wa RnB Damian Soul.
“Sina tatizo kabisa na hili jina ‘Bongo Fleva’, ni kitu kizuri kwa sababu kama kikisimamiwa kinaweza kuwa ni identity ya muziki ambao unatoka Tanzania.
“Tatizo ni kwamba limekuwa kama treni au basi ambalo kila mtu anaweza kudandia, awe na talent asiwe na talent.” Amesema Mwamba wa Kaskazini.
Amesema kwa hali hii wana hip hop wanaona kama ni shida kukaa kwenye bus moja na watu ambao hawana vipaji.
“Mtu unaona, aaagh..I’m in the same bus with someone...huyu ambae anaibia tu, unaona bora niachie, but Bongo Fleva is a good thing.” That’s Joh Makini.
Joh Makini ameshirikishwa na Damian Soul kwenye ngoma yake mpya ‘Ni Mapenzi’ iliyotambulishwa Jumanne (November 5) kwenye The Jump Off
0 comments:
Post a Comment