Meneja mpya wa klabu ya Man utd Louis van Gaal ametangaza msisitizo wa kutaka wachezaji watatu kusajiliwa na mashetani wekundu kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya soka nchini Uingereza August 16 mwaka huu.

Van Gaal, ambaye anatarajiwa kuwasili mjini Manchester juma hili ametoa agizo kwa viongozi wa klabu ya Man Utd kuhakikisha washambuliaji  Arturo Vidal, Angel Di Maria pamoja na  beki Mats Hummels wanasajiliwa haraka iwezekanavyo.

Meneja huyo kutoka nchini Uholanzi amesema anaamini hakuna linaloshindikana katika harakati za kuwasajili wachezaji hao watatu hivyo suala la kuwapata lipo mikononi mwa viogoni kwa kushirikiana na benchi la ufundi ambalo litakuwa chini yake.

Tayari mshambuliaji kutoka nchini Argnetina na klabu ya Real Madrid Angel Di Maria ameshaweka wazi dhamira ya kutaka kucheza soka katika ligi ya nchini Uingereza, ili hali mshambuliaji kutoka nchini Chile pamoja na klabu bingwa nchini Italia Juventus, Arturo Vidal yupo tayari kuondoka mjini Turine.

Kwa upande wa Hummels anayeitumikia klabu ya Borussia Dortmund, bado haijathibitika kama yu radhi kuondoka nchini Ujerumani kwa sasa.




0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About