“Hatukutaka watu wafahamu, tukaamua kukutana Marekani, mahali ambapo ilikuwa kazi sana kugundulika.”

MHISPANIOLA, Pep Guardiola, ameifanya Bayern Munich kuwa timu hatari zaidi msimu huu. Ameiweka kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Ujerumani, ameiingiza 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na leo Jumamosi anasaka taji la Klabu Bingwa ya Dunia wakati atakapomenyana na Raja Casablanca katika fainali nchini Morocco.
Baada ya kuinoa Barcelona kwa mafanikio makubwa kabla ya kujitoa kwenye timu hiyo alipochukua mapumziko ya mwaka mmoja, klabu kadhaa zilitajwa kumwania.


Katika orodha zilikuwamo timu vigogo nchini England, Manchester United na Chelsea. Lakini unafahamu Bayern Munich ilimnasaje? Subiri.


Rais wa Bayern Munich, Uli Hoeness, amefichua jinsi alivyomnasa Guardiola na kumfanya kuwa kocha wao baada ya kukutana naye Marekani alikokwenda kwa ajili ya biashara zake za kuuza soseji.

Hoeness anasema alifanya mazungumzo na kocha huyo wa zamani wa Barcelona mwaka jana alipokwenda Marekani kwa ajili ya biashara zake binafsi zinazoendesha familia yake.
Ilivyokuwa

Hoeness anabainisha alitumia fursa ya kwenda Marekani kibiashara na hivyo kutumia nafasi hiyo kuonana na Guardiola ambaye alikuwa mapumzikoni nchini humo na hivyo kufanya mkutano wa siri.

“Nilikuwa kwenye misafara ya biashara zangu binafsi,” anasema Hoeness, ambaye anaongoza kiwanda cha kutengeneza soseji.

“Nilienda Chicago kwanza kuonana na Aldi. Nilifahamu kwamba Pep alikuwa na mpango wa kurudi Barcelona kwa ajili ya mapumziko kidogo na kama tungeenda kukutana Hispania ingekuwa hatari.

“Hatukutaka watu wafahamu, tukaamua kukutana Marekani, mahali ambapo ilikuwa kazi sana kugundulika.”

Ferguson azidiwa ujanja
Wakati Hoeness anakwenda Marekani na kukutana na Guardiola, kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, alikuwa nchini humo pia kwa mapumziko yake aliposhuhudia mechi za mchezo wa tenisi.

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About