YANGA SC iliongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya mechi za kwanza za mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, kufuatia ushindi wa 5-1 dhidi ya Ashanti United, zote za Dar es Salaam.
JKT Ruvu ikapaaa kileleni baada ya mechi za pili na ikadumu hadi mzunguko wa tano ilipoipisha Simba SC. Angalau Simba SC ilidumu kwa muda mrefu huko hadi mzunguko wa 10, ilipozipisha Azam FC na Mbeya City.
Simba SC ikajivuruga na kujikuta inapotea kabisa ndani ya tatu bora, ikizipisha Azam, Mbeya City na Yanga SC.
Yanga ikarejea kileleni baada ya mechi za mwisho za mzunguko wa kwanza, kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya JKT Oljoro, huku Azam na Mbeya City zikitoshana nguvu kwa sare ya 3-3.
Pointi 28 zinaifanya Yanga iliyoanzia kileleni baada ya mechi za kwanza kumalizia kileleni pia, ikizizidi kwa pointi moja moja Azam na Mbeya City.

Vinara na watetezi; Yanga SC wamemaliza kileleni mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Bara

YANGA SC;
Ilianza Ligi vyema, lakini ikaingia kwenye wimbi la sare mfululizo, kabla ya kuzinduka na kufanya kweli, hatimaye kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni na wazi Yanga ipo katika nafasi ya kutetea ubingwa wake kutokana na ubora wa timu na wachezaji wake. Katika mechi 13, imeshinda nane, sare nne, imefungwa moja na Azam FC, imefunga mabao 31, imefungwa 11 na imemaliza na pointi 28
P W D L GF GA GD Pts
1 Yanga 13 8 4 1 31 11 20 28

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About