AGOSTI 24, 2013;
Juma Luizio amefunga bao la kwanza la msimu, dakika ya nne Mtibwa Sugar ikitoa sare ya 1-1 na Azam Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
AGOSTI 24, 2013;
Laurian Mpalile amekuwa mchezaji wa kwanza kujifunga dakika ya 23, Prisons ikifungwa 3-0 na Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
AGOSTI 24, 2013;
Aggrey Morris amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwa penalti, akiisawazishia Azam FC dakika ya 19 katika sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
AGOSTI 24, 2013;
Emmanuel Kichiba wa Ashanti United amekuwa mchezaji wa kwanza kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 12, timu yake ikifungwa 5-1 na Yanga
SEPTEMBA 18, 2013;
Amisi Tambwe amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick, akifunga mabao manne katika ushindi wa 6-0 wa Simba SC dhidi ya Mgambo JKT Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
SEPTEMBA 18, 2013;
Crispin Odula wa Coastal Union na Simon Msuva wa Yanga SC wanakuwa wachezaji wa kwanza kutolewa kwa pamoja kwa kadi nyekundu baada ya kugombana dakika ya 77, timu zao, zikitoka sare ya 1-1.
SEPTEMBA 18, 2013;
Kipa Abbel Dhaira wa Simba SC ametimiza mechi tatu za kudaka bila kufungwa hata bao moja, (Simba 1-0 JKT Oljoro, Simba 2-0 Mtibwa Sugar na Simba 6-0 JKT Mgambo).
SEPTEMBA 22, 2013;
John Bocco ‘Adebayor’ amefunga bao la mapema zaidi, sekunde ya 34, Azam ikishinda 3-2 dhidi ya Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
OKTOBA 13, 2013
Abdallah Juma anakuwa mchezaji wa pili kufunga mabao matatu peke yake katika mechi moja, Mtibwa Sugar ikishinda 5-0 dhidi ya JKT Oljoro Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
OKTOBA 20, 2013
Yanga SC walikwenda kupumzika wanaongoza mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC lakini kipindi cha pili walitepeta na kusawazishiwa mabao yote, hadi wakaomba mechi iishe, kwani kwa kasi ya Wekundu wa Msimbazi katika dakika za mwishoni, wangeweza kupata mabao zaidi.
OKTOBA 31, 2013
Simba SC v Kagera Sugar; Mechi hiyo ilihitimishwa kwa milipuko ya mabomu ya machozi, Polisi wakituliza ghasia, baada ya mashabiki wa Simba SC kuanza kung’oa viti kurusha uwanjani, kufuatia Kagera Sugar kusawazisha bao dakika ya pili ya muda wa nyongeza, baada ya kutimu dakika 90 na kupata sare ya 1-1.
NOVEMBA 1, 2013
Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga SC anavunja rekodi ya kipa Mganda Abbel Dhaira wa Simba SC kudaka mechi tatu mfululizo bila kufungwa, baada ya kudaka Yanga ikishinda 3-0 dhidi ya Rhino, 3-0 na Mgambo na 4-0 mbele ya JKT Ruvu.
NOVEMBA 7, 2013
Mwagane Yeya wa Mbeya City anafunga hatrick ya tatu ndani ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, katika sare ya tatu na Azam FC Uwanja wa Azam Complex.
NOVEMBA 7, 2013
Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga SC anaweka rekodi mpya msimu huu, baada ya kudaka mechi nne mfululizo bila kuruhusu nyavu zake kuguswa (Yanga 3-0 Rhino, 3-0 Mgambo, 4-0 JKT Ruvu na 3-0 JKT Oljoro).

10 Juu; Amisi Tambwe ndiye kinara wa mabao Bara mzunguko wa kwanza
0 comments:
Post a Comment