
Wimbo huu nimetumiwa na rafiki yangu Reuben Ndege. Kwa mujibu wa maelezo yake,wimbo huu naye ameupata kama “ajali” kupitia WhatsApp yake. Baada ya kuisikiliza akaona “ajali” hii ni nzuri na hivyo isiishie kwenye masikio yake tu.Nakubaliana naye. Ni wimbo unaoitwa Jisikie Nyumbani kutoka kwa msanii T-Boy. Bado hakuna details za kutosha kwamba umetengenezwa studio gani na producer wake ni nani. Zitakapopatikana details hizo tutaziongeza.
Nakubaliana na Reuben kwamba hii ni “ajali” nzuri kwa sababu achilia mbali kwamba ujumbe uliopo katika wimbo huu ni mzuri na wenye kuibua hisia za kizalendo, bali pia T-Boy ni msanii mwenye uwezo wa kuimba. Usikilize hapa chini,Jisikie Nyumbani na mpelekee mwenzako
0 comments:
Post a Comment