• YAFAHAMIKA - MESSI ANGEWEZA KUSAJILIWA NA CHELSEA KAMA MOURINHO ANGELIPA £105m.

  • Bobby Williamson kocha mpya Simba SC.

  • Njaa ya Ubingwa: Ligi Kuu Tanzania Bara.





Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.

Waliotupwa nje kutokana na tuhumua za ufisadi ni pamoja na Anna Tibaijuka- aliyekuwa waziri wa ardhi nyumba na makazi, Sospeter Muhongo-aliyekuwa waziri wa nishati na madini huku Lazaro Nyalandu akihamishwa kutoka wizara ya mali asili na italii aliyokuwa akihudumu.

Walioondolewa kwenye wizara zao za awali na kuhamishwa ni pamoja na Lazaro Nyalandu ambaye anarudi mazingira. Saada Mkuya Salum kutoka fedha na kuhamishiwa ikulu pamoja na Gaudensia Kabaka.Hayo ni baadhi ya majina niliyopata.

Aidha rais Kikwete amewaondoa baadhi ya mawaziri katika baraza lake kutokana na uwajibikaji hafifu ambao ni Chiza Christophera-kilimo, Maghembe Jumanne-maji, Hawa Ghasia-tamisemi na Mathias Chikawe-utumishi Kikwete pia amewaingiza wengine wapya kwenye baraza la mawaziri ambao ni Serukamba Peter, Deo Filikunjombe na Kigwangala Khamisi.Hao bado haijafahamika ni wizara zipi walizoteuliwa.

Pia wapo waliopanda cheo kuwa mawaziri kamili ambao ni Simbachawene George, Mwanri, Godfrey Zambi, Mwigulu Nchemba, January Makamba na Greyson Lwenge. Hawa taarifa kamili ya wizara watakazohudumia tutawaletea.

Inasemekana kuwa Kikwete amepangua na kulipanga upya baraza lake kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyotarajiwa. Pia atamteua mkuu mpya wa sheria wa serikali ndani ya siku tatu zijazo kama nilivyodokezwa.


Wema Sepetu azua gumzo kwenye mtandao baada ya kumuita Diamond
  • Wema Sepetu azua gumzo kwenye mtandao baada ya kumuita Diamond
  • Wema Sepetu azua gumzo kwenye mtandao baada ya kumuita Diamond
Huku macho na masikio ya wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania yakiwa kwenye bunge la katiba linalojadili lile sakata la tegeta ESCROW, mwanadada Wema sepetu ameamua naye kuzua gumzo kwenye mtandao baada ya kutoa salamu ya pongezi kwa kijana Naseeb al maarufu kama Chibu dangote ama Diamond platnumz kwa ushindi wake wa tuzo 3 kwenye tuzo za Channel O MUSIC AWARDS zilizofanyika huko Afrika ya kusini akitumia neno KAKA katika sentensi yake kitu ambacho kimezua minong’ono ya hapa na pale kwenye mtandao ule maarufu wa kijamii wa picha nchini.
Katika post yake hiyo Wema aliandika
 “…Hongera tele ziende kwa kaka platnumz... I must say he did Tanzania proud..”   na kufanya watu waanze kufunguka ya kwaio ya moyoni kuhusu kauli hiyo na baadhi yao walisema haya.

MELA : “Leo kawa kaka!!!!!! Aiseeee mapenz ya mastaa mafupi kama mkia wa kondoo”

“ LILY: “et kaka plutnums heheheheh wema bwana”

“PIERE: mara hii kaka tena?? Ohhhhhh”

ANNA: “hao ni wakuwaacha kesho.tu.watakua tena pamoja”
Katika tuzo hizo, diamond alisindikiwa na anayesemekana kuwa kipenzi chake cha sasa, mwanadada Zari ktukoa nchini Uganda, pamoja na mama yake mzazi na team ya wasafi.

Nini maoni yako mdau kuhusu ishu hii?


Karudi mzigoni: Angel di Maria amedai Real Madrid walimtumia barua katika siku ya mwisho ya fainali za kombe la dunia
ANGEL di Maria amedai kuwa Real Madrid walimuamuru asicheze mechi ya fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani.
Nyota huyo wa Manchester United aliyesajiliwa majira ya kiangazi kwa dau la paundi milioni 60 na kuvunja rekodi ya usajili nchini England amemlaumu rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwa kumuondoa katika michuano ya ulaya, akisisitiza kuwa hakuwa na nia ya kuondoka majira ya kiangazi mwaka huu.
Di Maria alikuwa hatari kukosa mechi ya fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani mwezi julai mwaka huu kwa majeruhi ya mguu, na ameweka wazi kuwa maamuzi ya yeye kutoikosa mechi hiyo yalifanywa na kocha wa Argentina, Alejandro Sabella, lakini Real Madrid walimuandikia barua wakimshauri asichezea.

Alipambana: Nyota wa Manchester United, Di Maria hatimaye alipangwa katika mechi ya fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani licha ya kuwa na majeruhi ya mguu

Kimataifa

1410046545686_Image_galleryImage_VERONA_ITALY_AUGUST_30_Ar
Siku zijazo: Manchester United  bado wanaiwinda saini ya  Arturo Vidal (pichani juu)
MANCHESTER United bado hawajamaliza matumizi makubwa ya fedha katika dirisha la usajili.
Katika dirisha dogo la usajili mwezi januari mwakani wametenga paundi nyingine milioni 50  kwa ajili ya kunasa saini za wachezaji wengine.
Tayari United imeshatumia paundi milioni 150 katika dirisha la usajili majira ya kiangazi jumlisha kumsajili Radamel Falcao.
Arturo Vidal, Mats Hummels na Sami Khedira ndio wachezaji wanaowaniwa zaidi na United.
Jaun Mata Garcia atauzwa mwezi januari kama sehemu ya kuongeza wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi cha Louis van Gaal.
Pia kuna taarifa kuwa mwanasoka bora wa dunia na Ulaya, Cristiano Ronaldo anaweza kurejea Manchester United.
Nyota huyo anayekipiga Real Madrid ana mapenzi makubwa na klabu yake hiyo ya zamani na anasema anaipenda toka moyoni.
On the move: United will look to sell Juan Mata as Louis van Gaal continues his rebuilding process
Atletico Madrid, Roma na Juventus  zipo tayari kumsajili Mata aliyesajiliwa na United kutoka Chelsea mwezi januari kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 37.
United inatarajia kukubali ofa ya paundi milioni 20.


 
 
Kutoka moyoni? Wakati bimkubwa Wema Isaac Sepetu akijiaminisha na kuhisi kuwa amepata mume ambaye ni baba bora, mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kuwa kamwe hafikirii kuoa, Ijumaa lina cha kukuhabarisha.
Wema Isaac Sepetu akiwa kwenye pozi la kimahaba na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Kauli hiyo ya Diamond inakuja wiki kadhaa baada ya Wema kuonekana na pete ya ndoa kidoleni kisha kukiri kuvishwa na ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva ambaye amerejea kutoka Marekani alikotwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki zilizokwenda kwa jina la African Muzik Magazine (AFRIMMA) 2014.
Hofu ya kuoa
Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalum, Diamond alisema kuwa anahofia kuoa kwa madai kwamba akifanya hivyo anaweza kuanguka kimuziki kitu ambacho hataki kimtokee maishani mwake.
Kumbe!
Jamaa huyo ambaye siku hizi anajiita Dangote (jina la tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote) alitiririka kuwa zamani alikuwa na wazo hilo la kuoa lakini akiwatazama wanamuziki wenzake waliooa mwisho wa siku, makali yao hupungua na wengine kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki.
Bofya hapa kumsikia Diamond
“Unajua unaweza kuona kama vile nazungumza kitu cha utani lakini ndiyo ukweli wenyewe.
“Kuna wanamuziki wengi walikuwa kwenye peak (kileleni) lakini walipooa tu ‘kiki’ yao ilishuka ghafla katika muziki na wengine wamepotea kabisa.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
“Ukifuatilia kwa umakini wapo mastaa wengi duniani ambao umri umekwenda sana lakini hawajaoa. Hata hapa nyumbani kuna mifano hai. Nadhani hofu yao ni kuona kuwa wakifanya hivyo watashuka kimuziki,” alisema Diamond.
Ni kweli kamvisha pete Wema?
Alipoulizwa kama ni kweli amemvisha pete ya uchumba Wema, msanii huyo hakuwa tayari kufafanua kwa kigezo kwamba pete ni urembo kama urembo mwingine kwa mwanamke.
Nje ya boksi
Baada ya kusikia msimamo wa Diamond, gazeti hili lilijiongeza na kutoka nje ya boksi ambapo lilizungumza na baadhi ya wasanii waliooa na wasiooa ambapo walieleza mambo mazito.
Jacqueline Wolper
Siri yafichuka
Katika mazungumzo yao kwa sharti la kutochorwa gazetini, wasanii hao walidai kwamba Diamond anahofia kupoteza kiki kwa warembo ambao wengi ndiyo mashabiki wake wanaoamini nao wanaweza kupata zali la kuolewa naye ndiyo maana humzingira na kumuomba namba ya simu kila anakokwenda.
Msururu wa mademu
Ilielezwa kwamba kwa kuwa jamaa huyo hupenda kuwa juu ndiyo maana alisharipotiwa kutoka na msururu wa wanawake mastaa ambao huchangia jina lake kuendelea kuwa juu.
Ilidaiwa kwamba wakati anatafuta namna ya kuchomoka kimuziki alidaiwa kutoka kimapenzi na warembo waliokuwa na majina madogo kama Rehema Fabian aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Miss Kiswahili.
Jokate Mwegelo.
Ilisemekana kwamba baada ya hapo alidaiwa kuwa na msururu wa wanawake mastaa kama waigizaji Jacqueline Wolper Massawe na Aunt Ezekiel Grayson na Jokate Mwegelo.
Baadaye jamaa huyo alidaiwa kuruka na wasichana ambao hawakuwa na kiki hivyo aliwamwaga ndani ya muda mfupi kama Najma na Natasha.
Baadaye Diamond alitua kwa Wema hadi akafikia hatua ya kumvisha pete ya uchumba mwaka 2012 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki jijini Dar.
Kumbukumbu zinaonesha kwamba muda mfupi baada ya kumvisha Wema pete ya uchumba walimwagana ambapo Diamond alitua kwa Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Irine Uwoya
Diamond hakudumu na Penny kwa madai kwamba mrembo huyo hakuwa na kiki kama ilivyokuwa kwa Wema ambaye jina lake halijawahi kushuka tangu alipovaa Krauni ya Miss Tanzania 2006/07.
Ilisemekana kwamba hata tuzo zilipungua ndipo akampiga Penny chini na kurudi kwa Wema ambaye inasemekana ndiye anayemng’arisha.
Hawa wameoa, je, wameshuka?
Baadhi ya mastaa waliooa ni pamoja na Mohamed Ahmed ‘Z-Anto’, Nurdin Bilal ‘Shetta’, Amini Mwinyimkuu, Lawrence Marima ‘Marlaw’, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ na wengineo.


Mtangazaji wa kipindi cha mahaba kiitwacho Ala za Roho kupitia Radio Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ hivi karibuni alilazimika kuyaanika maungo yake ya sehemu za mapaja kushuka chini baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mmoja wa mashabiki wake.Kupitia blog yake, Diva alidai kuwa siku za nyuma kuna mtu aliomba kuona sehemu hizo za mwili wake hivyo baada ya kumbania sana ameamua kumtimizia haja yake ili afurahi.

“Kuna mtu alikuwa akidai hajawahi kuona miguu yangu iko ikoje na kwamba nimekuwa nikionesha sehemu ya shingo tena kwa upande,leo nimeamua kumfurahisha,”alisema Diva. Sambamba na maneno hayo, mtangazaji huyo alijifotoa picha zilizoocha wazi sehemu kubwa ya mapaja yake kisha kuziweka kwenye ukurasa huo.

Diva ni mtangazaji mwenye sauti ya kimahaba, yenye uwezo wa kumtoa nyoka pangoni ambaye watu wengi wamekuwa na hamu ya kumuona jinsi alivyo kwani wamezoea kumsikia redioni tu.


 
 Diamond Platnumz  akionesha tuzo yake aliyoshinda kwa baadhi ya vyombo vya habari  na mashabiki waliofika kumlaki,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi(30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI




 Mwanamuziki nyota wa miondoko ya Bongo Fleva Diamond Platnumz akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.Pichani akilakiwa na Mama yake Mzazi na baadhi ya washabiki na wapenzi wa muziki huo.
 Diamond Platnumz akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014


Hiki  ndicho alichokisema:
"Haya sasa.....maelezo hatimaye yamepatikana....mnivumilie ni marefu Kidogo...! 
1. Pongezi kwa @officialalikiba nimesikia Mwana wa Dar es Salaam tu lkn kiukweli Mimi binafsi umenikonga moyo...! 
 
2. Ieleweke kwamba Mimi ni shabiki wa mziki mzuri hata ukiwa umeibwa na underground na wengi wenu mmekuwa mashaidi maana huwa na post video nikiimba miziki ya watu tofauti hata wasio mastar wakubwa...kwahyo mm sio shabiki wa mtu ni shabiki wa kazi ya mtu
3.Nimegundua wasanii wengi wa Tanzania tuna U mimi....hivi ulaya wangekuwa hvyo...Hollywood c kungekuwa na mtu mmoja tu au wawili basi....nadhani umefika muda wa wasanii Kama wasanii kila mmoja kujiamini ktk kazi Zake na kufikiria kufanya makubwa sio kufikiria kushindana na flani.....tena tukishirikiana tutaweza kufika mbali zaidi ya hapa...tutaendelea kila cku kuona maajabu wenzetu Nigeria wanafika mbali....wanajielewa na wanashirikiana...!Kama binadamu kukoseana kupo ila ukijua kosa kuomba msamaha na kuendelea na maisha ndo busara zaidi
 

 4.Hapa sasa....nieleweke jmn...Mashabiki wetu Tunawapenda sawa....lakini kwa namna moja au nyingine Mashabiki mnchangia bifu za wasanii....JAMANI Ukiwa shabiki wa Lulu haimaanishi umchukie Wolper(mfano)Kama ww ni shabiki wa mtu sio umchukie msanii mwingine na hii kwakweli ninaiona Tanzania tu(thou sio Mashabiki WOTE) 
5. Mwisho...WOTE tunategemeana wasanii tupendane tukiona wenzetu flani wana shida tusaidie kuondoa tofauti na Mashabiki pia nyie ndo msaidie kupatanisha watu sio kuchochea ugomvi....
Mungu alivyotuumba wengi alikuwa na maana yake sasa we ukitaka uwe Mkali pekeyako ungeumbwa mwenyewe ukawekwa kwenye dunia ya pekeyako tukusome kwenye history dunia flani Kuna mtu mkali yuko pekeyake..!duh nimechoka kuandika lkn cjamaliza.....bt I real wish wakali mngeungana mfanye mambo makubwa....naamini inawezekana...!"





Shilole si mgeni katika kuota vitu vikubwa. Kutoka kwenye ndoto yake ya kufanya kolabo na Jennifer Lopez, awamu hii ameenda mbali zaidi.
 Muimbaji huyo amechoka ‘Kuchuna Mabuzi’ na sasa anataka kuingia mjengoni. Mrembo huyo ambaye jina lake halisi ni Zuwena Mohamed, amepanga kugombea ubunge kwenye jimbo analotokea la Igunga mkoani Tabora katika uchaguzi wa mwaka 2015!

Akizungumza kwenye kipindi na Sizi Kitaa cha Clouds TV, Shilole amesema yupo serious na nia hiyo na kama Mungu akipenda atakuwa mbunge wa jimbo hilo.
 
“Baada ya Dokta Dalali Kafumu anayefuata ni mimi,” amesema Shilole. 

 “Mimi nadhani napenda jimbo langu na napenda wakazi wangu wa Igunga wananiona toka nakua mpaka sasa hivi, kwahiyo wanafurahi. Sasa wananiambia ‘sisi hatutaki kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa wananipa changamoto. 

"Vitu viwili vya kwanza ambavyo nitavifanya nikiingia kwenye lile bunge nikiwa kama msanii, kwanza nitatetea haki za wasanii, cha pili Igunga yangu wapo wakazi wa Igunga vijana wapate kazi, yaani akina mama, wale mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. Kwahiyo nitawatafutia kazi, nitajenga chuo cha muziki,” alijinadi muimbaji huyo.
 
“Mimi jimbo langu nalijua na nimekua pale mpaka nimekuwa mkubwa lazima nilitimize sitaki wananchi wangu wapate tabu. Mimi nadhani wanaoenda kugombea majimbo yasiyo ya kwao wanaweza fanya chochote, lakini kama ni wa hapo lazima itakuuma. 

"Lakini unakuta mtu wa Dar es salaam anakwenda kugombea Mtwara huko nani anamjua? Mimi nitaenda kugombea kwangu lazima nitapata kura lazima watanipa! Kwahiyo kaeni tayari Shilole ni mbunge mtarajiwa Igunga,” alitamba.


 Kweli mfadhii mbuzi binaadam atakuuzi wewe ommy D leo ndo wa kumsupport dully na kumuacha Alikiba aliekutoa na Nai Nai??Ulipokuwa unataka utoke vipi ulitafuta mtu wa 
kukutoacna ukajua ni Ally Kiba sasa hivi unamuona mavii khaaa binaadam hapana hata kama ume base upande mmoja but usische mbachao kwa msala upitao ndo maana watu wengine maendeleo cyenu yanaishia chalinze kwa roho mbaya


Ni mwendo wa vipaaaaaaaara!!!!!....


Miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa bongo fleva wiki hii ni pamoja na kusikia kauli ya Alikiba kuhusu chanzo cha beef kati yake na msanii mwenzake Diamond Platnumz.

Kupitia kipindi cha Sporah kilichoruka July 22 Clouds TV, Alikiba amefunguka mambo mengi ikiwemo jinsi walivyofahamiana kwa mara ya kwanza, chanzo cha beef yao na wakoje hivi sasa.

Kabla hujafahamu undani wa alichokizungumza, hizi ni facts chache alizozitoa Alikiba katika Interview hiyo.

1.Alikiba ndiye alimpa ruhusa Bob Junior amrekodie Diamond nyimbo zilizomtoa kama ‘Kamwambie’ katika studio yao ya Sharobaro!
2.Alikiba alishirikishwa katika wimbo wa Diamond ‘Lala Salama’!
3. Alikiba ni shabiki wa nyimbo za Diamond hadi sasa!
4. Diamond aliomba ashirikishwe katika hit ya Alikiba ‘Single Boy’!
5. Alikiba ana watoto watatu, lakini hana uhusiano tena na mama zao

Asilimia kubwa ya kipindi ilihusu uhusiano wa Alikiba na Diamond, na hii ni sehemu ya maelezo ya Kiba.

Alikiba aliizungumzia sababu iliyozaa beef kati yake na Diamond, swali la Sporah lilikuwa kama Alikiba ana namba ya simu ya Diamond:

“Nilikuwa nayo kipindi Fulani, nilipohisi amenikosea nikaona sina ulazima…kuna kipindi alinikosea kwasababu nilisikia amesema kwamba tulirekodi wote ile nyimbo ya ‘Single Boy’, na si kweli. Halafu anasema mimi ndio nilimfuta…

kwa kunikosea kwa Diamond nilihakikisha kutokana na mimi mwenyewe ndo nilifanya nyimbo yake ‘Lala Salama’ iko kwenye album yake, akanifuta nikahisi amenikosea sana nilichoimba mimi akawa ameimba yeye, alichonituma nifanye nimefanya kwa mapenzi yote, na mimi namsupport kila msanii wa Tanzania anayefanya vizuri anayeimba vizuri, sikatai anaimba vizuri sijui ukisema ame copy am proud, mi sijamaind wala nini lakini usiseme kwa watu ukadanganya ukaonekana mi sifai, siko hivyo mimi.”

Aliendelea,
“Watu wengine ambao hawaelewi vizuri wanaweza wakamwamini Diamond, kila mtu ana mapenzi yake labda kuna wengine wanampenda Diamond wengine wanampenda Alikiba. wanaweza wakawa wengine wanampenda Diamond wakaamini mimi nimemfuta Diamond kwenye nyimbo ya ‘Single boy’ lakini mimi wala, shahidi producer Manecky ndo alitengeneza ile nyimbo. Sikuwahi kwenda na Diamond kwenye studio na sikuwahi kufikiria kufanya nyimbo nae.

Ila alinipigia simu baada ya ile nyimbo kuleak, imevuja Single boy, tayari nimeshafanya na Jaydee, akaisikia kwenye simu Ali kuna nyimbo nimeisikia unaonaje ile tukifanya ile itakuwa safi sana afu akanipa mpaka idea ya video na nini, nikamwambia sawa inawezekana lakini mimi nadhani itapendeza zaidi tukifanya nyimbo nyingine mimi na wewe,kwasababu hii tukifanya mimi na wewe haita make sense inapendeza ikiwa single boy single girl, hicho ndo kitu nilimjibu.
Akaniambia poa lakini we fikiria hiyo, nikamwambia okay lakini hata kama nikifikiria mi sioni jibu hapo, jibu ni hilo hilo. Hicho ndo kitu ambacho nilimjibu Diamond. Baada ya kama wiki moja nikaja kusikia kwenye mablog, mpaka nikapigiwa simu kwamba mimi nimemfuta kwenye ile nyimbo wakati yeye ndio aliyenifuta katika nyimbo yake, shahidi producer wangu mimi KGT anaitwa ambaye nimetoka naye muda mrefu sana..nyimbo zangu zote alikuwa akiproduce yeye”.

Kuhusu nani aliyemuita mwenzake kwaajili ya wimbo ambao Alikiba anadai Diamond alimfuta (Lala Salama)

“Hakuna aliyemuita mwenzake, ila mimi pale studio ambayo alikwenda kurekodi Diamond ni studio ya kwangu mimi ambayo ilikuwa imenitoa pale G-Records na watu wote wanajua nimetokea pale. ..Nakwenda kutembea kama nyumbani , kuwatembelea studio kumtembelea producer wangu, nikamkuta Diamond nae studio anarecord. Kuingia pale ndani ya studio nikakuta amesha record kabisa…akaniambia hebu sikiliza hii, nikasikiliza nikamwambia umeimba vizuri sana…nikajaribu kumwambia ungeimba hivi na hivi na hivi ingekuwa vizuri sana ila niliheshimu mamuzi yake kwasababu kila mtu na style yake, nikawa nataka kuondoka akaniita, akaniambia nakuomba uingize zile sauti zako za juu, kila mtu anajua ukisema hivyo, kuna sauti zangu flani hizo silaha zangu naweza kusema wengi wanapenda.

Nikamwambia nikiingiza vile nitaharibu mi nahisi umeimba vizuri sana, akaniambia imba bwana, atleast chochote kile, ndio nikaimba sasa mimi pale baada ya kufanyaje, nimeona aibu kumkatalia mbele ya producer wangu. Ni Kwa mapenzi yote nilifanya, nikamfanyia vizuri, kweli nilikwenda na feeling nzuri sana kwasababu nyimbo ilikuwa ndio style yangu vile vile.

Lakini sasa, kwasababu hata producer wangu hakuniambia nikaja kuisikia nyimbo imetoka ameingiza yeye vile nilivyokuwa nikiimba mimi yaani njia nilizokuwa nimepita akaingiza yeye, kwahiyo nikahisi kama amenifanya mtoto wakati mimi ni mkubwa wake na anajua hilo”.

Baada ya Alikiba kugundua hilo alichukua hatua gani za kumuuliza Diamond au producer?

“Niligundua kabisa producer wangu kunipigia simu mimi ilikuwa sio sawa kwasababu ile nyimbo sio yake halafu nilimpa tu uhuru wa kufanya kazi na kila msanii na nilijisikia vizuri Diamond amekuja mpaka pale studio kwetu kufanya kazi ..
Mi nilichukua simu yangu nikampigia Diamond, alichonijibu akasema yeye mwenyewe hajui , basi mi nikaachana na haya mambo, from then nikaona hamna tatizo lakini kwa kujua yeye alinifuta katika nyimbo yake”.

Alikiba na Diamond walivyofahamiana:

“Unajua mimi Diamond nimemjua muda mrefu sana, mimi ndio nimemrelease pale akafanya nyimbo Sharobaro wakati mimi niko kwenye tour America, nilikuwa pale kama president, vice wangu alikuwa Bob Junior ambaye ndio producer pale, akanipigia simu kwasababu hakuwa na maamuzi ya kumruhusu arekodi, bana kuna msanii anaitwa Diamond anaimba vizuri tu, nikamwambia kama anaimba vizuri mrekodie”.

Alikaba amekiri kuwa ni shabiki wa nyimbo za Diamond lakini si shabiki wake:

“Mimi sijutii, vile vile am happy kwa yeye kufanikiwa kufanya kazi nzuri, amerepresent nchi yetu anajitahidi kwasababu honestly naweza kusema ukweli mimi pia sometimes nakuwa shabiki wa music..mimi sio shabiki wa Diamond. Unapoongelea shabiki unaweza kushabikia nyimbo basi, kuna nyimbo ambazo amenifurahisha Diamond ameimba nikasema yes amefanya vizuri, lakini sio kwamba namshabikia yeye, mi napenda music, sikufichi mi naskiliza music ya kila msanii anayeimba vizuri, siwakubali wasanii napenda kazi zao”.

Kuhusu alivyojipanga kurudi kwenye game na kukabiliana na Diamond ambaye kwa sasa ndie msanii aliye juu zaidi:

“Kizuri kikikosekana kibaya pia kinaonekana kizuri…!!”

Sporah alimuuliza kuwa haoni kwa kipindi alichokaa kimya Diamond ndio kama amechukua nafasi yake kwenye muziki:

“Hakuna mtu aliyechukua nafasi yangu, labda kama ni kiti ambacho nilikuwa nimekaa kinavumbi na nachotakiwa ni kukipangusa tu na kukaa tena, lakini labda yeye yuko siti nyingine ila the back seat. Formula tofauti najua sasa hivi wanahitaji nini sababu muda ambao nimepumzika nilikuwa kama mshabiki wa muziki…lakini sikuweza kupata muziki ule kama tulikuwa tukisikia zamani Latifah…Violet ambao ule kama wimbo wa taifa. Na nimeona wanamiss kwasababu mafans wangu kwa upendo wao kwakweli nawashukuru sana kwa mapenzi ambayo wamenionesha uvumilivu na kunikumbusha Ali njoo we need you…and kwa respect ambayo nimewapa nawaambia Alikiba himself anakuja tena very soon, now new material, new look, na next level kila kitu”.

Ujumbe wa Alikiba kwa mashabiki wake:

“Asabteni tena na tena (mashabiki) malalamiko yenu nimepata sana, samahani najua nimewa letdown, kama mlivyoona wengine wamepata chance ya kushine na wakatuwakilisha kwasbabu tu Alikiba aliwaachia nafasi hiyo…narudi tena very soon so get ready for this na mnipokee vizuri.”

Siku mbili zijazo Alikiba ataachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Mwana Dar es salaam’.Stay tuned! ‘mwenyekiti’ chake ndo kaishakipangusa vumbi so wengine waende chumbani wakalale? (na watuache tulale) LOL!

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About