
KOCHA wa Holland Louis van Gaal amesisitiza kuwa shujaa wake wa penalti kipa Tim Krul (pichani) bado atakuwa kipa namba 2 kwenye mechi ya nusu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Argentina Julai 9.
Kipa huyo wa Newcastle aliingizwa sekunde za lala salama kwenye mechi ya kifo ya robo fainali dhidi ya Costa Rica iliyofanyika katika mji wa Salvador.
Na kama alivyotarajiwa Krul akaokoa penalti mbili na kuivusha Holland kwa matuta kwenda hatua ya nusu fainali.
Lakini licha ya ushujaa huo, Van Gaal amesema kipa wa Ajax Jasper Cillessen ataendelea kuwa namba wani.
0 comments:
Post a Comment