BAO pekee la dakika ya 113 kupitia kwa kungo Mario Goetzelimeiwezesha Ujerumani kutwaa ubingwa wa kombe la dunia 2014.


Argentina iliyocheza kwa kujihami zaidi, huku ikionekana wazi kusubiria hatua ya matuta, ikajikuta inalala 1-0 na kufanya historia ya fainali ya mwaka 1990 iliyozikutanisha timu hizo, ijirudie.

Kwa sehemu kubwa ya mchezo, Ujerumani walitandaza soka maridadi na kwa hakika imevuna ushindi iliostahili.

Uchawi wa Lionel Messi haukuweza kuisaidia lolote Argentina ambapo alidhibitiwa vizuri na safu ya ulinzi ya Ujerumani.

Kwa Messi na Muller kushindwa kufunga mchezo huu, mshambuliaji wa Colombia, James Rodriguez mwenye mabao sita, anakuwa ndiyo mfungaji bora wa kombe la dunia.

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About