Furaha: Kroos, akiwa na mpenzi wake Jessica Farber
Kimeeleweka: Ndivyo unavyoweza kusema na tayari Real Madrid imeonekana kuwa ndiyo sehemu sahaihi kwa kiungo wa kimataifa wa Ujeumani Toni Kroos. Kroos ameeleza kwamba anaondoka Bayern Munich baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la Dunia na sehemu sahihi kwake ni Real Madrid.
Kroos, 24 alikuwa muhimu katika kikosi cha Joachim Low nchini Brazil.
Na, wakati akishangilia ushindi wa 1-0 dhidi ya Argentina kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia, Kroos alithibitisha kwamba atajiunga na miamba ya La Liga.

Dili limekamilika: Toni Kroos amethibitisha kwamba atajiunga na Real Madrid baada ya kukubaliana
Furaha: Kroos, akiwa na mpenzi wake Jessica Farber
'Tumemaliza fainali za Kombe la Dunia kwa furaha. Sasa nakwenda Madrid, hivyo ndoto mbili zimefanikiwa,' Kroos aiiambia UOL.
Kiungo huyo wa kati anatarajiwa kupokea mshahara wa paundi 160,000 kwa wiki akiwa Bernabeu huku Bayern ikiridhika kumuachia kwa uhamisho wa paundi 20 million na Kroos amekubali mktaba wa miaka mitano na mabingwa wa Champions League.
0 comments:
Post a Comment