Nahodha wa Brazil Thiago Silva amefungiwa, hivyo Dante anatarajiwa kuhodhi nafasi yake, lakini Luis Gustavo amemaliza adhabu yake. 


Neymar ni majeruhi hivyo Brazil wanaweza kuwatumia viungo watatu wa kati au wanaweza kumchagua kiungo mshambuliaji mmoja kati ya Willian au Bernard. 
Kocha wa Ujerumani Joachim Low lazima afanye uamuzi wa busara kumuita mlinzi wa kati Per Mertesacker, ambaye hakucheza kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Ufaransa huku kikosi hicho kikiripotiwa kutokuwa na majeruhi. 
Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Estadio Mineirao, mjini Belo Horizonte. 

BRAZIL V UJERUMANI

Uso-kwa-uso 
  • Brazil na Ujerumani zimecheza mechi nyingi za Kombe la Dunia kuliko timu nyingine (102 na 104), lakini zenyewe zimekutana mara moja tu kwenye Kombe la Dunia. Hiyo ilikuwa kwenye fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2002, ambapo Brazilwalishinda 2-0.
  • Pia wamekutana mara tatu wakianza na sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kirafiki mwaka 2004, Brazil ikashinda 3-2 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali mwaka 2005 na Ujerumani ikashinda 3-2 kwenye mchezo wa kirafiki mwaka 2011. Michezo yote hiyo ilifanyika kwenye ardhi ya Ujerumani.
  • Brazil imefunga katika kila mchezo kati ya michezo yao 10 ya mwisho kukutana, wastani wa magoli 2.2 kwa kila mchezo.
Brazil 
  • Brazil imefanya failo nyingi zaidi dhidi ya Colombia (31) ni nyingi zaidi kuwahi kufanywa na Brazil kwenye mashindano ya Kombe la Dunia tangu data hizo zilipoanza kukusanywa mwaka 1966.
  • Wamepoteza mchezo mmoja kati ya michezo 26 na walifungwa na Switzerland August mwaka jana (W19, D6, L1).
  • Hawajafungwa katika michezo 42 mfululizo waliyocheza nyumbani, huku kipigo cha mwisho kukipata ilikuwa kutoka kwa Paraguay August 2002.
  • Brazil imeingia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa mara 11, ingawa hii ya leo itakuwa nusu fainali yao ya nane (kwa sababu ya mifumo tofauti ya mashindano ya awali).
  • Nusu fainali pekee kupoteza ilikuwa nusu fainali yao ya kwanza dhidi ya Italia mwaka 1938. Imeshinda mara tano na kutoka sare mara moja - na sare hiyo ilifuatiwa na penalti ambapo waliifunga Uholanzi mwaka 1998.
  • Mshambuliaji wa Brazil aliyeumia Neymar amechangia 50% ya magoli 10 ya Brazil katika Kombe la Dunia (amefunga magoli manne na kutengeneza moja).
Ujerumani 
  • Ujerumani (ikijumuisha Ujerumani Magharibi) imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia mara 13, ingawa hii itakuwa nusu fainali ya 12 (waliingia nusu fainali ya mwaka 1974 wakitokea katika nafasi ya pili kwenye kundi).
  • Ujerumani ni nchi ya kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa mara nne mfululizo.
  • Katika nusu fainali 11, wameshinda mara nne, wamefungwa mara tano na sare mbili - na michezo ya nusu fainali waliyotoka sare kwenye muda wa kawaida walishinda kwenye matuta.
  • Ujeumani hawajafungwa kwenye michezo 16 ya kimataifa (W11, D5), ni rekodi nzuri kuliko timu yoyote kwenye Kombe la Dunia.
  • Ujerumani (matatu) imefungwa magoli machache zaidi kuliko nchi yoyote kwenye Kombe la Dunia. Ni Ghana na Algeria ndizo zimefanikiwa kuipenya ngome ya Ujerumani.
  • Miroslav Klose anaweza kucheza mchezo wa 23 wa Kombe la Dunia kama atapangwa leo, rekodi inashikiliwa na Lothar Matthaus (mechi 25). Paolo Maldini pia amecheza michezo 23 ya Kombe la Dunia.

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About