MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeamuru Kamati Kuu ya Chadema kutojadili
suala la uanachama wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto katika
mkutano utakaofanyika leo Dar es Salaam.
Hatua hiyo inatokana na kesi ya madai iliyofunguliwa na Zitto dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Willbrod Slaa.
Jaji John Utamwa aliamuru Zitto asijadiliwe katika mkutano huo hadi uamuzi wa ombi lake alilowasilisha mahakamani, litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Alitoa uamuzi huo jana jioni baada ya kutupilia mbali pingamizi la awali, lililowasilishwa na Chadema, ikiomba ombi la Zitto lisisikilizwe kwa kuwa lina makosa kisheria, hata hivyo alisema sababu za kukataa pingamizi hilo atazitoa leo.
Alisema Chadema wanaweza kuendelea na mkutano, lakini wasijadili suala la Zitto na kuahirisha kesi hiyo hadi leo, ambapo Zitto atawasilisha kiapo kinzani na ombi lake la msingi litasikilizwa.
Ombi lake
Ombi lake
Katika ombi lake, Zitto aliiomba Mahakama iamuru kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachofanyika leo, kisijadili suala lake la uanachama hadi Baraza Kuu la Chama litakaposikiliza rufaa yake.
Aidha, aliomba Mahakama imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa ampe nakala za mwenendo wa vikao vilivyomvua uongozi ili aweze kukata rufaa.
Zitto kupitia kwa wakili wake, Albert Msando, alifungua kesi hiyo ya madai jana chini ya hati ya dharura, ikasajiliwa kwa namba moja ya mwaka huu na kupangiwa Jaji na kuanza kusikilizwa mchana.
Zitto kupitia kwa wakili wake, Albert Msando, alifungua kesi hiyo ya madai jana chini ya hati ya dharura, ikasajiliwa kwa namba moja ya mwaka huu na kupangiwa Jaji na kuanza kusikilizwa mchana.
Hata hivyo, mawakili wa Chadema, Tundu Lissu na Peter Kibatala, waliwasilisha pingamizi la awali wakiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo, kwa kuwa ina dosari kisheria.
Wakili Kibatala alidai kuwa Zitto alikosea kutumia vifungu vya sheria katika kufungua kesi hiyo kwa kuwa alivyotumia havihusiani.
Aidha, hati ya kiapo inayounga mkono kesi hiyo ina upungufu wa kisheria kwani ina maoni, jambo ambalo ni kinyume cha sheria inayosimamia hati za viapo.

Kwa upande wake, Lissu alidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kimakosa, kwa sababu migogoro ya chama, dini na michezo haiwezi kupelekwa mahakamani, inatakiwa kutatuliwa ndani ya taasisi husika, kulingana na taratibu na Katiba.
Aliongeza, kuwa migogoro inaweza kufikishwa mahakamani iwapo mwanachama hatapewa haki ya kusikilizwa, lakini katika hati ya kiapo ya Zitto ameeleza kuwa amepewa barua ya kuitwa na Kamati Kuu ili akasikilizwe.
“Kama kapewa barua ina maana Kamati Kuu imempa haki ya kumsikiliza, kwa nini afungue kesi kama hafanyi ‘forum shopping’ kwa kuwa anahofia uamuzi wa kesho (leo)?” Alihoji Lissu.
Mwigamba afunguka
Mwigamba afunguka
Mwigamba akizungumza na gazeti hili jana alisema alikuwa anajua ambacho kingefanyika leo kwamba atafukuzwa uanachama, lakini kabla ya uamuzi huo wa Mahakama alikuwa tayari kufika mbele ya Kamati Kuu kuhojiwa kama barua ilivyomtaka.
Alisema alichokuwa nacho kama kingetekelezwa, bila Mahakama kuzuia asingekuwa na mpango tena na siasa wala kuhamia chama chochote bali angerejea kwenye shughuli zake za uchumi alizodai zimeyumba baada ya kujikita kwenye siasa.

Akizungumza kwa simu huku akiweka bayana kitakachomwondoa Chadema, Mwigamba alisema: “Nimejiandaa kwenda kesho (leo) kwenye Kamati Kuu, nipo tayari kujitetea kwa kile nitakachohojiwa, lakini lazima watu wajue matokeo yalishaandaliwa, kwani suala la kujieleza ni lingine na hatua itakayochukuliwa ni jambo lingine pia.
“Uamuzi tayari naujua, nakwenda kuhojiwa kutimiza wajibu, nimeitetea sana Chadema, mimi si kichaa kuvuruga nilichokijenga, sisi wa chini tunapambana kukijenga chama lakini wajuu wanakivuruga, najua walichokipanga kesho (leo) kwa kuwa tayari wajumbe wanaitwa mmoja mmoja kutengenezwa, watakachofanya kesho ni kuweka muhuri wa walichokiamua sasa,” alisema Mwigamba.
Alipoulizwa kwa nini afikirie kufukuzwa wakati kikao bado hakijaamua hivyo, alisema: “Ninazungumza haya kwa uhakika, ipo mifano hai, mwenzagu wa Mara (Mwenyekiti wa Chadema, Bathlomeo Machage) na wenzake walifukuzwa, baada ya baadhi ya viongozi kusema wazi kwenye mikutano ya hadhara, kuwa watang’olewa na kweli Kamati Kuu ikawafukuza.
“Ukiacha hilo, juzi juzi nilipofanyiwa fujo Arusha na kupigwa kama mwizi, Lema (Mbunge wa Arusha) aliendesha mikutano ya hadhara na aliwahakikishia wananchi kuwa sitarudi, Lema alishasema hili mara nyingi, hata Mbunge wa Karatu, Israel Natse amesema katika mkutano wa hadhara lazima tufukuzwe, kwa kuwa sisi ni wasaliti katika chama”.
Aliendelea kusema kuwa Lema na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje kwa nyakati tofauti katika mikutano kadhaa ya hadhara waliendelea kusisitiza kuwa Chadema itawashughulikia na kuwahakikishia wananchi kwa viapo kuwa lazima “tupigwe chini”.
Imeandikwa na Gloria Tesha na Flora Mwakasala

0 comments:
Post a Comment