Posted by Unknown on 10:55 with No comments
Posted by Unknown on 08:30 with No comments

Jarida la Glitz Africa limetoa orodha ya wasichana 20 warembo zaidi barani Afrika (20 Most Beautiful Women in Africa) ambapo hata hivyo imetawaliwa na wanawake wa Nigeria na Ghana.
Ni Happiness Millen Magese pekee amekuwa mwanamke kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kuingia kwenye orodha hiyo.

Orodha nzima ni hii:
Leila Lopes (Angola), Vimbai Mutinhiri (Zimbabwe), Oluchi Orlandi (Nigeria), Yvonne Nelson (Ghana), Dillish Mathews (Namibia), Agbani Darego (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria), Stephanie Linus (Nigeria), Genevieve Nnaji (Nigeria), Joselyn Dumas (Ghana), Yvonne Okoro (Ghana), Jackie Appiah (Ghana), Millen Magese (Tanzania), Omotola. Jalade-Ekeinde (Nigeria), Zainab Sheriff (Sierra Leone), Naa Okailey Shooter (Ghana), Nadia Buari (Ghana), Lerato “Lira” Molapo (South Africa), Babalwa “Barbz” Mneno (South Africa), Elham Wagdi (Egypt).
Posted by Unknown on 08:28 with No comments

Hakuna Afrika nzima; Basi jipya la wachezaji wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, lililowasili nchini juzi likiwa tayari kusafirishwa visiwani Zanzibar ambako timu hiyo imekwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi.
Hili ni aina ya mabasi ambayo yanatumiwa na klabu za Ulaya kama Manchester United, Bayen Munich na Barcelona ambalo kwa Afrika Azam inaweza kuwa klabu ya kwanza kulimiliki.

Kitu cha maana

Kila siti ina TV

Kuna friji

Kuna choo
Posted by Unknown on 20:19 with No comments

Ujumbe wa kutoka nchini Cameroon wanatarajiwa kwenye nchi Ulaya kuwashawishi wachezajiwa wa nchi hiyo wanachezea katika nchi za ulaya kujiunga na timu ya taifa ya nchi hiyo "Indomitable Lions".
Mpango huo wa kusaka vipaji vipya umekuja wakati Cameroon ikiwa inajiandaa kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka kesho nchini Brazil.
Chama cha soka cha Cameroon - Fecafoot kimesema mpango wao kwa sasa ni kushawishi wachezaji wanne wanaocheza soka ya kulipwa nchini Ufaransa.
Wachezaji hao Axel Ngando anachezea klabu ya Auxerre ya ligi daraja la pili nchini Ufaransa, Samuel Umtiti anachezea Lyon na Jean- Christophe Behebeck anachezea Valenciennes.
Mchezaji mwinginie anayewindwa ili kuuongeza nguvu kwenye timu ya taifa ya Cameroon ni Paul Geoges Ntep de Madiba ambaye pia naye anayechezea Auxerre ya Ufaransa.
Tunataka kuwashawishi hao wachezaji wachezee timu ya taifa ya Cameroon, na hasa kwenye fainali za Kombe la Dunia na pia wachezee Cameroon kwa hapo baadae Shirikisho la soka la Cameroon limesema kwenye taarifa yake.
Posted by Unknown on 20:15 with No comments
ULIKUWA NI MWAKA WA ATHUMAN IDD ' CHUJI'
Na Baraka Mbolembole
Athumani Idd ' Chuji' , sahau kuhusu umri wake, kiungo huyu wa ulinzi na mashambulizi wa klabu ya soka ya Yanga, amepitia vipindi vingi vigumu katika maisha yake ya soka. Akianzia soka lake katika timu ya Polisi Dodoma, 2005, Chuji alitokea kuwa mlinzi bora wa kati katika soka la Tanzania, alikuwa akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika timu ya taifa ya vijana ' Serengeti Boys' mwaka huo, akitokea timu za nje ya Dar es Salaam. Kupata nafasi ya moja kwa moja katika timu ya taifa ukitokea mkoani, bila shaka wewe utakuwa mchezaji ' asiyegusika' popote pale.
Namba tano mwenye sifa za utulivu, mpangaji mzuri wa ngome na kiongozi mwenye kujiamini, ni sifa ambazi zilimfanya Chuji kusajiliwa na Simba, kwa ajili ya msimu wa mwaka 2006. Chuji, 25 kwa sasa ( umri huu ndiyo unaotambulika' aliingia Simba na kukuta wachezaji wengine wazuri kama yeye. Katika nafasi ya ulinzi wa kati ambayo alikuwa akicheza katika timu ya Polisi Dodoma, ndani ya Simba, nafasi hiyo ilikuwa chini ya Victor Costa, na beki Mrundi, Said Koko'o hivyo ilimfanya kukutana na upinzani mkali wa kuwania nafasi.Athumani Idd ' Chuji' , sahau kuhusu umri wake, kiungo huyu wa ulinzi na mashambulizi wa klabu ya soka ya Yanga, amepitia vipindi vingi vigumu katika maisha yake ya soka. Akianzia soka lake katika timu ya Polisi Dodoma, 2005, Chuji alitokea kuwa mlinzi bora wa kati katika soka la Tanzania, alikuwa akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika timu ya taifa ya vijana ' Serengeti Boys' mwaka huo, akitokea timu za nje ya Dar es Salaam. Kupata nafasi ya moja kwa moja katika timu ya taifa ukitokea mkoani, bila shaka wewe utakuwa mchezaji ' asiyegusika' popote pale.
CHUJI WA KADI ZA MARA KWA MARA....
Hata aliporudi uwanjani baada ya kumalizika kwa adhabu yake, Chuji alikuwa ni mchezaji wa kiwango kilekile, akizima kila kitu kuhusu tabia yake kucheza soka la ukosefu wa nidhamu kwa kiwango chake na mchezo uliochangamka. Moja kati ya majuto makubwa ya aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Marcio Maximo ni adhabu ya mchezaji huyo. Akiwa mfuasi ya nidhamu ni wazi Maximo alikuwa akitambua mchango wa Chuji katika kati yake. Tabia yake mbaya ilimfanya kuingia katika vifungo vya mara kwa mara, na hivyo kukosa nafasi ya kuichezea timu ya taifa mara kwa mara.
SAHAU YOTE, ALITUPELEKA CHAN
Kiwango kizuri cha Chuji, kilionesha ni kwa nini kocha Maximo alipinga adhabu yake wakati ule, 2007. Chuji alikuwa sehemu muhimu ya wachezaji wa timu ya taifa waliozisukuma nje, Kenya, Uganda na Sudan kisha kutinga kwa michuano ya CHAN, 2009, nchini Ivory Coast. Alifunga moja ya mabao bora wakati Stars ikiifunga, Sudan katika mchezo wa mwisho wa kufuzu, jijini Dar, kabla ya kwenda kusaidia ushindi wa kukumbukwa ugenini, jijini Khartoun.
CHUJI APOTEZA DIRA....
Wakati kiwango chake kiliposhuka zaidi, 2009. Chuji aliishia kugombana na kocha Maximo katika timu ya taifa. Makocha wa klabu yake, Dusan Kondic, na baadaye, Kostadin Papic bado walikuwa wakisema kuwa hakuna kiungo kama Chuji katika nyakati za sasa nchini. Baadae kiwango kilizidi kuporomoka huku mambo ya nje ya uwanja yakimuathiri kimchezo, akashuka thamani hata kwa mashabiki wake mwenyewe. Alitumia misimu miwili kuanzia 2009- 10, na 2010 - 11 akicheza soka huku akiitwa ' mzee'. Kisha baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Yanga, klabu haikumuongeza tena mkataba. Akarudi Simba, na kusajili katika michuano ya Kagame, 2011. Akaishia kucheza dakika zisizozidi kumi wakati timu yake ikicheza michezo sita hadi fainali.
NITAENDELEA KUMUHUSUDU PAPIC KWA HIKI...
Hata wakati, Chuji akiitwa 'mzee' katika utawala wake Yanga, kocha Papic bado aliendelea kusema kauli yake ile ile kuwa Chuji ni kiungo wa aina yake. Baada ya kumalizika kwa michuano ya Kagame, Simba iliamua kumtema Chuji, na hivyo akajikuta nje ya soka kwa muda wa miezi sita. Kila mtu alikuwa akisema lake, wapo waliokuwa wakisema kuwa mwisho wake umefika na kuna wakati akakanusha taarifa za yeye kutumia madawa ya kulevya ndiyo sababu ya kutemwa kwake Simba. Baada ya Sam Timbe kufukuzwa kazi ya ukocha, Yanga ilimrejesha Papic na kocha huyo akaamua kumpatia mkataba wa miezi sita ndani ya Yanga.
Akafanya vizuri na kupewa mkataba wa miaka miwili zaidi, na mapema mwezi uliopita alirefusha kwa miaka miwili zaidi ya kuendelea kuichezea Yanga. Kwa sasa, amepevuka zaidi na amekomaa kimaamuzi. Si mkorofi akiwa uwanjani, ana jiheshimu na kuheshimu mchezo wenyewe. Amekuwa kiongozi, na mchapakazi mzuri kwa timu. Kama ni safari, Chuji amepitia safari ndefu, ila kwangu nampa tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu kwa kipindi cha mwaka mzima, 2013. Amefanya kazi yake vizuri. Ningemrudisha Chuji katika nafasi ya ulinzi wa kati ili anisaidie katika timu yangu. Nafasi hii inahitaji busara zaidi, na pengine hata Dos Santos angemrudisha katika nafasi aliyomtoa. Beki tano.
Posted by Unknown on 19:57 with No comments

NGWE ya lala salama ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 unatarajia kuanza kushika kasi januari 25 mwakani.
Kwasasa timu zote 14 zinazoshiriki ligi hiyo zipo katika maandalizi ya vikosi vyao ili kufanya vizuri zaidi ya mzunguko wa kwanza.
Wataalamu wengi wa soka wanasema mzunguko wa pili kama ilivyo kawaida timu zinajigawa katika makundi matatu.
Kundi la kwanza linajumuisha timu zinazowania ubingwa, wakati kundi la pili ni lile la timu zinazowania nafasi za katikati ambazo si nzuri sana wala mbaya sana, cha msingi katika nafasi hizi, timu zinakuwa katika mikono salama.
Kundi la tatu ndio balaa, hapo kunakuwepo na timu zinazopigana kushuka daraja, hivyo zinashindana kwa nguvu zote kusaka ushindi wa kuwasogeza mbele.
Ukiangalia msimamo wa ligi kuu mpaka sasa wakati tunasubiri mzunguko wa pili, timu za kundi la kwanza unaweza kusema ni Vinara Yanga, Azam fc, Mbeya City, pamoja na Simba sc.
Simaanishi nyingine haziwezi kuingia katika nafasi hizo. Mpira wa miguu ni mchezo wa hadharani, hivyo baadhi ya timu zikiwemo Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, na Ruvu Shooting zinaweza kuingia katika mbio za kuwania ubingwa endapo zitachanga vyema karata zao.
Msimamo uko hivi; Yanga wapo kileleni kwa pointi 28, nafasi ya pili wapo Azam fc na pointi zao 27, nafasi ya tatu wapo Mbeya City wakijikusanyia pointi 27, huku nafasi ya nne ikishikiliwa na simba SC yenye pointi 24. Timu hizi zinakamilisha timu nne za juu `Big Four` wakati mzunguko wa pili unasubiriwa.
Nafasi ya tano inakaliwa na Mtibwa sugar wenye pointi 20, sawa na Kagera Sugar katika nafasi ya sita, lakini Mtibwa wana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Nafasi ya saba wapo Ruvu shooting wakiwa na pointi 17, wakati nafasi ya nne inashikiliwa na wagosi wa kaya, Coastal Union kwa pointi 16, nafasi ya tisa wapo JKT Ruvu na pointi zao 15, huku nafasi ya kumi ikishikiliwa na Rhino Rangers ya Tabora yenye pointi 11.
Kibarua kipo nafasi nne za mwisho ambapo JKT Oljoro wameshikilia nafasi ya 11 kwa pointi 10 sawa na Ashanti United nafasi ya 12, tofauti ni wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Nafasi ya 13 wapo Tanzania prisons wakiwa na pointi 9, huku Mgambo JKT waikiburuza mkia kwa pointi 6 tu.
Kwa msimamo huu utagundua kuwa nafasi za juu zinaonekana kung`ang`aniwa na timu za Yanga, Azam fc, Mbeya City pamoja na Simba sc. Lakini Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na Ruvu Shooting zinaweza kuingia katika kinyang`anyiro cha ubingwa. Sio hizo tu, hata timu nyingine kama Coastal union, Ruvu Stars zinaweza kupanda juu kutegemeana na matokeo ya timu zilizopo mbele yao.
Mzunguko wa pili utakuwa na ushindani mkubwa sana kwa timu zinazowania ubingwa. Ukiangalia hali zao kiuchumi, morali kubwa, ubora wa wachezaji, mipango yao na makocha waliopo, utagundua kuwa kibarua kitakuwa kizito.
Kwa kifupi tuangalie baadhi ya mabadiliko yaliyopo katika timu nne za juu na maandalizi yao kuelekea mzunguko wa pili.
YANGA SC
Timu hii ipo katika maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.
Kwa bahati Mbaya kumetokea mabadiliko ya benchi la ufundi ambapo Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia Disemba 22 mwaka huu.
Kwa maana hiyo, Yanga wanahaha kupata kocha mpya kuelekea mzunguko wa pili. Ukipiga hesabu za muda uliobakia kufikia januari 25 na februari ambapo wataanza kampeni za ligi ya mabingwa barani Afrika, utagundua kuwa kocha mpya atakuwa na kazi nzito kuandaa kikosi, na mbaya zaidi akija na falasafa mpya ya uchezaji.
Lengo sio kuingia kiundani zaidi kuhusu suala hili la kumfukuza kocha ambalo yawezekana ni udhaifu wa viongozi wa Yanga au ni uhalisia wa jinsi kiwango cha timu yao kinavyoshuka siku hadi siku licha ya kusheheni nyota kibao.
Yanga kwasasa wapo chini ya kocha msaidizi, Fredy Felix Minziro na wanajiandaa kwenda kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajia kuanza kushika kasi januari mosi mwakani katika uwanja wa Amaan mjini Unguja na Gombani kisiwani Pemba.
Michuano hii itakuwa muhimu sana kwa Yanga, kwani itawapa nafasi ya kupima uwezo wa kikosi chao kabla ya kuanza kutetea ubingwa wake na kushiriki michuano ya kimataifa.
Kuna uongezeka la wachezaji wapya katika kikosi chake, hivyo unaweza kukubaliana na mimi kuwa kutakuwa na mabadiliko ukilinganisha na mzunguko wa kwanza, lakini endapo atapatikana kocha mwenye ubora wa juu.
Ongezeko la Juma Kaseja, Hassan Dilunga na Emmanuel Anord Okwi, yawezekana kutawapatia nguvu kubwa zaidi na kuendelea kufanya vizuri.
Kaseja ana uzoefu mkubwa sana na ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa. Okwi naye ni mchezaji bora kwa wakati wote, lakini Dilunga ni chipukizi na anahitaji muda zaidi wa kujiweka sawa katika soka la ushindani.
Kwa usajili wa Okwi, Yanga inafikisha wachezaji watano wa kimataifa, wengine ni Mbuyu Twite, Didier Kavumbagu, Haruna Niyonzima na Hamis Friday Kiiza. Wachezaji hawa wapo katika kiwango kizuri, ingawa bado wameonekana kutokuwa na makali barabara.
Pia imesheheni wachezaji wazawa wenye kiwango cha juu ambao ni pamoja na Juma Kaseja, David Luhende, Nadir Haroub `Canavaro`, Kelvi Yondan `Vidic`, Athuman Idd `Chuji`, Frank Domayo, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa , kipa Ally Mustapha `Bartez`, Deo Munish `Dida` na wengineo.
Ukiangalia majina ya wachezaji wa Yanga kulinganisha na timu nyingine kama Mbeya City, Ruvu Shooting hata Simba Sc, unaweza kuamini kwa asilimia mia moja kuwa Yanga watashinda mechi zote.
Hakika hakuna ushindani wa majina kabisa, Yanga wanaonekana kuwa na kila aina ya mchezaji, lakini kumbuka mpira wa miguu ni mchezo wa mipango na unachezwa hadharani na ndio maana wakiwa na wachezaji wao bora, walifungwa mabao 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba yenye wachezaji wengi vijana.
Kwa kikosi cha Yanga, anahitajika kocha wa kuunganisha timu ili wacheze kitimu. Kama atapatikana mwalimu mzuri, bila shaka Yanga watafanya vizuri ngwe ya pili nap engine kutetea ubingwa wao. Cha msingi tusubiri muda ufike.
SIMBA SC
Simba wakiwa chini ya kocha Abdallah Kibadeni walianza mzunguko wa kwanza vizuri na kuongoza, japokuwa walikuja kupoteza mwelekeo na kuishia nafasi ya nne.
Waliamua kufanya mabadaliko ya benchi la Ufundi ambapo Kibadeni pamoja na msaidizi wake, Jamhuri Kiwhelo walitimuliwa na mikoba yao kuchukuliwa na Mcroatia Zdravko Logarusic `Loga` akisaidiwa na Seleman Matola `Veron`.
Mbali na kubadili benchi la ufundi, pia wameongeza nguvu katika dirisha dogo ambapo wamewasajili, Ivo Mapunda, Yaw Berko, Donald Mosoti, Awadh Juma Issa, Ali Badru pamoja na kumrejesha Uhuru Seleman Mwambungu aliyekuwa akicheza kwa mkopo Coastal Union ya Tanga.
Mapunda, Awadh, Mosoti, Uhuru, walicheza mechi ya nani mtani Jembe ambapo waliunganisha nguvu zao na wachezaji wengine wakiwemo, Gerrard Jonas Mkude, Ramadhan Singano `Messi`, Said Ndemla, Betram Mwombeki, Hamis Tambwe, Joseph Owino Gella na wengine.
Katika mechi hiyo, Simba ilicheza vizuri na kuonekana kuimarika. Na sasa inajiwinda na mashindano ya mapinduzi yanayotarajia kuanza kushika kasi januari mosi.
Endapo Simba watatulia na kocha wao na kuongeza nguvu zaidi ya mechi ya Nani Mtani Jembe, basi hapana shaka watarudi mchezoni na kuendelea kutafuta ubingwa wa ligi kuu, ikizingatiwa wanazidiwa pointi nne tu na Yanga waliopo kileleni.
AZAM FC
Klabu hii imeachana na kocha wake , Mwingereza Sterwart John Hall na kuanza maisha mapya na kocha raia wa Cameroon, Joseph Marius Omog.
Wanakwenda Zanzibar kutetea ubingwa wao wa kombe la Mapinduzi. Pia watatumia michuano hiyo kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu bara pamoja na michuano ya kombe la shirikisho mwakani.
Katika dirisha dogo la usajili, Azam fc wamemuongeza mshambuliaji mmoja kutoka Ivory Coast, Mouhamed Kone.
Bila shaka baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza, benchi la ufundi lilijiridhisha na uwezo wa wachezaji wake kikosini.
Klabu hii yenye makazi yake Mbande, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, imekuwa ikishindana kwa misimu mitatu mfululizo.
Msimu wa 2011/2012 walikuwa wanashindana na Simba katika mbio za ubingwa na kujikuta wakiambulia nafasi ya pili. Msimu wa 2012/2013, Simba wakajitoa, kibarua kikabaki kwa Azam fc na Yanga na wakaishia nafasi ya pili.
Msimu huu wapo katika mbio za ubingwa, Simba wapo nyuma yao, wanapambana na Yanga pamoja na Mbeya City.
Ukiangalia mfululizo wa kufanya vizuri kwa Azam, japokuwa hawajafanikiwa kutwaa ubingwa, utajiridhisha kuwa wamekuwa wapambanaji wa kweli na bila shaka wataendelea na kasi yao chini ya kocha mpya, Omog.
Yanapotokea mabadiliko ya kocha, kuna mambo mawili; Moja, timu inaweza kuongeza kiwango na pili inaweza kupoteana endapo wachezaji watashindwa kuenda sambamba na falsafa ya mwalimu.
Kwasasa ni mapema kuwatabiria lolote, tunaamini wanatambua nini cha kufanya na ndio maana wapo katika maandalizi kabambe.
Mzunguko wa pili, Azam fc wanaweza kuendana na kasi ya ushindani.
MBEYA CITY
Hii ni timu ngeni ligi kuu. Msimu huu ni wa kwanza kushiriki michuano hii mikubwa, lakini wameonesha ukomavu mkubwa na kuleta changamoto kali mzunguko wa kwanza.
Hakuna timu yoyote iliyoweza kupata pointi tatu mbele ya Mbeya City chini ya kocha wake Mzalendo, Juma Mwambusi akisaidiwa na Maka Mwalwisyi.
Waliungana kwa dhati na mashabiki wao waliokuwa wanawafuata popote pale wanapoenda. Wachezaji walikuwa na morali kubwa na kuucheza mpira kwa kasi kubwa, umakini na malengo ya ushindi.
Walifanikiwa kushinda nyumbani na ugenini na hivyo kuamsha ari kwa wapenzi wengi wa soka hususani jijini Mbeya.
Kwasasa wapo katika maandalizi ya mzunguko wa pili na bahati nzuri wamepata nafasi ya kucheza mapinduzi Cup kwa mara ya kwanza.
Hii itawajenga zaidi kwani watakutana na mazingira tofauti na bara. Watacheza na timu za Zanzibar pamoja na timu za Kenya na Uganda.
Itakuwa nafasi nzuri kwao kujipima uwezo wao kuelekea mzunguko wa pili ligi kuu bara.
Cha kufurahisha hakuna mabadiliko ya kikosi chao, lakini wamemuongeza mchezaji mmoja tu ambaye ni Saad Kipanga.
Ni ngumu kusema Mbeya City wataendeleza makali yao, lakini inawezekana kutegemeana na maandalizi yao, motisha kwa wachezaji na mipango ya ndani na nje ya uwanja.
Lakini bado nawatabiria kufanya vizuri kutokana na kusheheni wachezaji wenye kasi kama Deus Kaseke, Mwagane Yeya, Paul Nonga, Peter Richard, Jeremiah John, Alex Seth na wengine wengi.
Ni suala la kusubiri muda ufike ili tuone maujanja yao. Pia mapinduzi itaonesha wazi kama wana mwelekeo japokuwa itakuwa sehemu ya kujaribu kikosi chao.
Kukutana na timu za Tusker, AFC Leopard, KCC na URA itakuwa changamoto nzuri sana achilia mbali Simba, Yanga na Azam ambazo tayari wameshakutana nazo ligi kuu.
Baada ya kuangalia timu nne za juu, kwa nafasi za katikati huwa hazina ushindani sana kwani timu hzi huwa zinakuwa na uhakika wa kubakika ligi kuu kwa msimu unaofuata.
Timu nyingine kama ilivyo kwa timu za juu, zimefanya usajili katika dirisha dogo kama ifuatavyo;
ASHANTI UNITED
Ndiyo inayoongoza kwa wachezaji 15 ambao ni Kassim Kilungo, Mohamed Banka, Bright Obinna, Victor Costa, Juma Mpongo, Juma Jabu, Ally Kondo, Shafii Rajab, Mohamed Faki, Abubakar Mtiro, Patrick Mhagama, Ally Kabunda, Hassan Kabuda, Idd Ally na Rahim Abdallah.
RUVU SHOOTING; Ally Khan na Jumanne Khamis,
RHINO RANGERS; David Siame, John Kauzeni, Salum Mamlo, Jingo Seleman, Darlington Enyinna, Rajab Twaha, Godfrey Mobi na Mussa Digubike.
TANZANIA PRISONS; Dennis Liwanda, Godfrey Pastory, Henry Mwalugala, Jamal Salum na Brayton Mponzi.
OLJORO JKT; Jacob Masawe, Mansour Ali, Juma Mohamed, Amour Mohamed, Mohamed Ali, Mussa Nahoda, Benedict Ngasa, Seleman Makame, Shija Mkina, Ali Omar na Shaweji
MGAMBO SHOOTING; Suleiman Khatib, Bolly Ajali, Amri Sambinga na Issa Ali.
JKT RUVU; Chacha Marwa, Sino Augustino, Idd Mbaga na Cecil Luambano.
Coastal Union, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar hazijafanya usajili kutokana na kuviamini vikosi vyao.
Timu zote zimeshaanza mipango ya mazoezi, kinachosubiriwa ni muda muafaka kufika.
Kulingana na usajili wa timu hizi, labda tunaweza kupata kitu kipya kutoka kwao, lakini timu zinazoshika nafasi za mwishoni zitakuwa na kibarua kizito zaidi.
Mgambo Jkt, Tanzania Prisons, Ashanti United na JKT Oljoro zinatakiwa kujipanga zaidi ili kuepuka mkasi wa kushuka daraja.
Baadhi ya timu za mkiani, zimeanza harakari za kujinasua na mtego wa kuporomoka daraja, hivyo kwa kuanzia, zimebadili makocha wao.
Prisons imepata kocha mpya David Mwamwaja, Ashanti United, Abdallah Kibadeni, na JKT Oljoro imnasa Hemed Morroco.
Mabadiliko haya yamelenga kuzinusuru timu hizi na tayari zote zimeshaanza mazoezi na kambi kujiwinda na mzunguko wa pili ambao utakuwa wa mapambano ya kufa na kupona.
Tusubiri kuona matunda ya mabadiliko haya, na inawezekana zikaja na sura mpya au zikazidi kwenda shimoni.
Posted by Unknown on 07:25 with No comments

Awadh Juma (kulia0 mmoja wachezaji sita wapya wa Simba.
KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekutana Jumamosi (Desemba 28, 2013) kujadili mambo mbalimbali yaliyofikishwa mbele yake ikiwemo usajili wa dirisha dogo ambapo klabu zenye matatizo zimepewa hadi Januari 10 mwakani kurekebisha.Taarifa ya TFF, imesema baadhi ya klabu ikiwemo Simba zimezidisha idadi ya wachezaji, hivyo zimepewa hadi muda huo kupunguza ambapo zikishindwa kazi hiyo itafanywa na Kamati yenyewe.Simba ina nafasi tano za kujaza kwenye dirisha dogo lakini imewasilisha majina ya wachezaji sita.
Pia klabu nyingine zimetakiwa ama kuvunja mikataba ya wachezaji au kuendelea kuwa nao, na si kuendelea kuwalipa mishahara wakati imeshawaondoa katika orodha yao.
Kuhusu mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyesajiliwa Yanga, TFF imesema inafahamu kuwa klabu ya Simba bado haijalipwa fedha za kumuuza klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na itasaidia kufuatilia FIFA fedha za mauzo ya mchezaji huyo.
Posted by Unknown on 07:19 with No comments
Huku mchumba’ke, Penniel Mungilwa ‘Penny’ akifungasha virago kurejea kwao, mzee mzima Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza kumuoa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Awali kabla ya kufikia eneo la kutangaza kuoana, Diamond aliweka wazi jukwaani kwamba yeye na Wema wamerudiana.
Baada ya shoo hiyo iliyomalizika saa moja usiku, paparazi wetu alimfuata Diamond akiwa amesimama na Wema na kuwauliza kama kweli wana nia ya kufunga ndoa. “Hilo mwana mbona lipo wazi, nataka kumuoa staa na nataka kuzaa na staa,” alisema Diamond huku Wema akiwa hapingi.
Awali kabla ya kufikia eneo la kutangaza kuoana, Diamond aliweka wazi jukwaani kwamba yeye na Wema wamerudiana.
Baada ya shoo hiyo iliyomalizika saa moja usiku, paparazi wetu alimfuata Diamond akiwa amesimama na Wema na kuwauliza kama kweli wana nia ya kufunga ndoa. “Hilo mwana mbona lipo wazi, nataka kumuoa staa na nataka kuzaa na staa,” alisema Diamond huku Wema akiwa hapingi.
Posted by Unknown on 07:09 with No comments
Wachezaji wa timu ya Clouds Media Group wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mtanange wa kufunga mwaka dhidi ya timu ya magorikipa wanaocheza Ligi Kuu ya soka tanzania Bara.
Mbwiga akijifua.
Mbwiga akijifua.
Kocha mchezaji wa timu ya Clouds Media Group, Mbwiga Mbwiguke (kulia) akiwaongoza wachezaji wenzake katika mazoezi.
Wachezaji wa timu ya Makipa wanaocheza Ligi Kuu wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Makurumla jijini Dar es Salaam.
Mchezajki swa timu ya Makipa, Ivo Mapunda akisalimiana na Shaffih Dauda.
Kikosi cha Clouds Media Group
Timu ya Makipa wa Ligi Kuu wakiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa tizmu ziote mbili wakisimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha kocha wa makipa wa timu ya Simba, Marehemu James Kisaka.
Mchezaji wa timu ya Makipa Shaban Kado akimiliki mpira huku Bakari Masuli (kulia) akijaribu kumzuia.
Said Saleh 'Mbwiga Mbwiguke' (katikati) akitafuta mbinu za kumpokonya mpira Ivo Mapunda.
Mbwiga Mbwiguke (kushoto), akichuana na golikipa wa Mtibwa Sugar Hussein Sharif ''Cassilas''.
Mbwiga Mbwiguke (kushoto), akichuana na Hussein Sharif.
Mbwiga akimtoka kipa wa Yanga Deogratius Munishi 'Dida'.
Mshambuliaji wa Clouds Media Group, Maulid Kikucha akimiliki mpira mbele ya golikipa wa JKT Ruvu Said Mohammed.
Beki wa Clouds Media Group, Said Tully akimiliki mpira huku akizongwa na Hussein Sharif.
Hekaheka......
Mbwiga akifanya mahojiano na Juma Pondamali na Abdulhalim Humud.
Huniwezi......
Said Mohamed akimtoka mchezaji wa Clouds Media.
Posted by Unknown on 15:16 with No comments
Ni msanii gani anayecheza ligi moja na Diamond Platnumz sasa hivi? Naamini yupo kwenye ligi yakemwenyewe na hadi sasa hana mpinzani. Japokuwa kama ni mpira wa miguu, Diamond anaweza kuwa kwenye ligi kuu pamoja na timu zingine (wasanii wenzie) kwa anachokifanya, anaweza kuwa kwenye ligi kuu plus ambayo hakuna msanii mwingine anayefikia matawi yake.
Kutoka kwenye historia ndefu iliyokumbwa na umaskini wa kutupa enzi za utoto na ujana wake kabla hajatusua, hadi kufikia kuwa msanii tajiri, anayetafutwa kuliko wote kwaajili ya show na anayelipwa fedha nyingi zaidi kuliko wote. Kutoka kwenye maisha ya kudhauliwa, kufanya kazi kwenye viwanda na ujira wa shilingi 3,000 kwa siku, hadi kuwa msanii anayeingiza si chini ya shilingi milioni 40 kila wiki. Hakuna msanii anayependwa zaidi nchini kwa sasa kumzidi.
Pamoja na sifa nzuri za kuwa hitmaker maisha yake upande wa pili yamekuwa yakiandamwa na scandal nyingi. Amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana wengi warembo na wenye majina ambao wengi wao ameishia kuwavunja roho kutokana na kutokuwa mwaminifu kwenye uhusiano wake.
Japo anasema amewahi kuumizwa sana na Wema Sepetu aliyemtuhumu kwa kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao, Wema pia anasema amewahi kuumizwa mara nyingi na Diamond. Kwa maana nyingine ni kuwa, Diamond na Wema wana mambo mengi wanayofanana; wote ni heartbreakers.
Wema na Diamond wamekuwa na uhusiano wa on and off kwa kipindi kirefu. Pamoja na wakati mwingine kila mmoja kuamua kuendelea na maisha yake, wapenzi hawa wameendelea kuhook up kisirisiri na kuendelea kulila tunda lao. Mara ya kwanza wameachana, Wema ndiye aliyemshutumu mwenzi kwa kumsaliti.
“Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate,” Wema aliliambia gazeti la Mzuka katikati ya mwaka huu. “Nilikuwa sijui and maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari nimesharidhika naye.
Nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza. Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka, nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi pamoja akanikutana napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, tukachuniana, sikulala mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona ile hali lakini hataki kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo zangu nikaenda kwa dada yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha akaendelea na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu.”
Kipindi Diamond anakutana na Jokate, mrembo huyo alikuwa tayari yupo kwenye uhusiano na mchezaji wa ligi ya NBA, Hasheem Thabeet. Uhusiano wao ulikuwa umedumu kwa miaka miwili na Jokate alikiri kuwa alikuwa akimpenda sana mchezaji huyo. Hata hivyo muda huo umbali wao na matatizo ya hapa na pale ukamfanya Jokate awe kwenye hali ya upweke na hivyo kumpa nafasi Diamond.
“Kulikuwa na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi. Ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini angenitongoza mwaka huu nisingemkubali,” Jokate aliliambia gazeti la Ijumaa Wikienda October mwaka huu.
Hata hivyo, Jokate alijikuta miongoni mwa wasichana wengi waliyoumizwa na Diamond baada ya kuwa naye kwa kipindi cha miezi miwili tu.
Kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, cha katikati ya mwaka huu, Diamond alikiri kumuuliza Jokate.
“Kwasababu alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea,” alisema Diamond.
Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”
Bongo5 iliwasiliana na Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli ya Diamond na kusema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli. “Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” alisema Jokate.
Pamoja na kuachana huko kulikoonesha ishara ya kutorudiana tena, Diamond na Wema waliendelea kuwa na ukaribu ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa ukiwaumiza wengi. Msichana aliyekuja kuumizwa zaidi ni Penny ambaye kwake Diamond alikuwa mwanaume wa kipekee.
“Lakini I will tell you one thing, Diamond is an amazing person, whatever you see anachofanya, whether he is kissing, he is talking to me, whether ananichekesha, yaani he is a five star. So you can imagine ilikuaje. It was weird but very good; everything about him is just amazing,” Jokate aliliambia jarida la Mzuka.
Aliliambia jinsi ambavyo Diamond alikuwa akimfanyia surprise nyingi na mapenzi tele.
“The first one I think is buying me a car coz sikuexpect, I didn’t see it coming, ilikuwa out of the blue. Unajua tumeshazoea kwamba watu wanaofanya vitu hivi ni wanaume wakubwa, wababa mpaka uhongwe umehongwa na mtu mzima lakini for Diamond amesema hivyo tu ghafla…. nilikuwa sijui natoka naenda wapi akaniambia hebu njoo nikuambie he said, ‘I got you a car, he gave me money akasema go and buy that car,” alisema na kuongeza kuwa Diamond alimkabidhi shilingi milioni 15 kununua gari hilo.
“He said go buy this car. Ananiulizaga, he is very funny’ unapenda gari fulani mi’ mimi najibu yeah I like it’. I was so shocked, ghafla so I think that’s the first surprise. He is too sweet; kwanza he will come take you out for a dinner out of the blue. Yaani anafanya vitu ambavyo kwa age yake na persona yake vilivyo alivyo an artist unategemea awe ghetto, ‘ebwana uko wapi twenzetu pale tukapige kiepe’ unajua vile. But he is very sweet that surprises me, he surprises me I think every day. Na anachonisurprise kingine kikubwa I will tell you guys, ni uwezo wake wa kufikiri, he is very smart.”
Bahati mbaya kuamini huko kumekuja kugeuka baada ya hivi karibuni Diamond kurudiana na Wema Sepetu na ukweli huo ulibainika baada ya kuvuja picha zao wakiwa Hong Kong hivi karibuni. Tukio hilo liliuvunja vibaya moyo wa Penny ambaye tayari alikuwa akiishi na Diamond na nyumbani kwao alikuwa akijulikana na mchumba aliyepitishwa na familia nzima akiwemo mama yake Diamond na dada zake.
Usaliti huo ulipelekea mgogoro mkubwa kati ya Diamond na Penny ambaye kuna tayari kuna tetesi kuwa wameshaachana rasmi. Tangu hapo Wema amekuwa haoni aibu kuonesha mapenzi yake kwa Diamond ikiwa ni pamoja na kupromote show ya Diamond ya Christmas.
Kwenye show hiyo ya Jumatano hii ndipo mambo yalipowekwa wazi zaidi ambapo Wema alikuwa mmoja wa watu waliopanda kwenye stage na kuongea na watoto waliokuwa wakishuhudia show. Kwenye show hiyo Diamond alisikika akiuliza: Mnataka kumjua mchumba wangu”? Baadaye wakati akitaka kuimba wimbo wake ‘Ukimwona’, hitmaker huyo aliuliza tena: Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani,” na ndipo Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.
Baada ya Penny, hatujui ni msichana gani atakayevunjwa tena moyo na Diamond kutokana na kuendelea kwa uhusiano usiokatika na Wema kama vile wamekula yamini.
Posted by Unknown on 22:20 with No comments
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MAANDALIZI ya kombe la Mapinduzi linalotarajia kuanza kutimua vumbi januari mosi mwakani yanakwenda vizuri na timu zote zilizothibitisha kushiriki zinatarajia kuwasili desemba 31 mwaka huu.
Msemaji wa kamati ya mashindano , Farouk Karim amesema kuwa timu za Tusker fc, AFC Leopard za Kenya, KCC, URA za Uganda , Simba sc, Yanga, Azam fc na Mbeya City za Tanzania bara tayari zimeshathibitisha kushiriki na kamati ya maandalizi imeshakamilisha taratibu za kuzipokea.
SIMBA imepangwa kufungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kucheza na AFC Leopards ya Kenya Januari Mosi wakati Yanga wakishuka dimbani siku inayofuata kuikabili Tusker FC.
Karim amesema mgeni rasmi katika mechi ya ufunguzi itakayopigwa januari mosi majira ya saa mbili usiku katika uwanja wa Aman kisiwani Unguja baina ya Simba sc dhidi ya AFC Leopard ya Kenya atakuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italia, Cesare Prandelli.
Pambano la Simba na Leopards litatanguliwa na mechi kati ya wenyeji KMKM na KCC ya Uganda litakalopigwa saa 10 jioni kwenye uwanja huohuo.
“Ninavyozungumza na wewe muda huu, Prandelli yupo hapa Zanzibar mapumzikoni na tayari amekubali kufungua michuano hii yenye maana kubwa katika miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar”. Alisema Karim.
Karim alisema katika michuano ya mwaka huu viwanja viwili vitatumika ambavyo ni Gombani kisiwani Pemba na Aman Kisiwani Unguja.
“Uwanja wa Gombani upo katika hali nzuri na unavyojua una nyasi za bandia. Uwanja wa Aman umefanyiwa ukarabati mkubwa na hivi sasa wataalamu kutoka China wapo hatua za mwisho kabisa kukamilisha shughuli yao”. Alisema Karim.
Mratibu huyo alitoa wito kwa wadau, wapenzi wa soka visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi kwani kamati ya mashindano inategemea mapato ya milangoni kufanikisha mipango.
“Michuano hii inagharimu zaidi ya shilingi milioni 600, hatuna fedha hizo, tunategemea mapato ya milangoni, hivyo mashabiki kufika kwao kwa wingi ndio mafanikio yetu”. Aliomba Karim.
Aidha ameziomba taasisi na makampuni ya bara na visiwani kujitokeza kufanya matangazo katika michuano hiyo ili angalau wapate pesa za kuendeshea michuano hiyo.
Michuano iliyopita, Azam fc walitwaa ubingwa, lakini mwaka huu kuna changamoto mpya hasa kutokana na uwepo wa timu za Dar Young Africans na Mbeya City ambazo hazikushiriki.
Mechi zote za hatua ya makundi na robo fainali zitafanyika kwenye viwanja wa Gombani Pemba na Aman Unguja, wakati nusu fainali na fainali zitapigwa kwenye Uwanja wa Amani.
Katika michuano iliyopita Simba waliishia nusu fainali baada ya kuondolewa na Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 2-2 hata baada ya kuongezwa dakika 30.
Posted by Unknown on 22:06 with No comments
Dayna Nyange Msanii kutoka Morogoro amelalamikiwa na Msanii Mwenzake
kutoka Kigoma aitwae Vumbe wa K Town
kwa kuiba Wimbo Wake uitwao
Pendo na Yeye Kuibadilisha na kuiita Mimi na Wewe.
Kupitia account yake ya facebook hichi ndicho alichoandika Vumbe wa K Town
juu ya Dayna.
''Wimbo wa Dayna uitwao Mimi na Wewe ni Wimbo wng nae kaamua kufanya malipiz
kwangu badala ya Diamond..Tokea umetoka leo ndio nimeusikia huu wimbo ni moja kati ya
nyimbo mbili nilizompelekea kwa niaba aziskize ipi angeweza kufanya vzr
ilikua hiyo ambayo mm niliita "Pendo" na "wapo"ambayo ndani alikua na
kutoka Kigoma aitwae Vumbe wa K Town
kwa kuiba Wimbo Wake uitwao
Pendo na Yeye Kuibadilisha na kuiita Mimi na Wewe.
Kupitia account yake ya facebook hichi ndicho alichoandika Vumbe wa K Town
juu ya Dayna.
''Wimbo wa Dayna uitwao Mimi na Wewe ni Wimbo wng nae kaamua kufanya malipiz
kwangu badala ya Diamond..Tokea umetoka leo ndio nimeusikia huu wimbo ni moja kati ya
nyimbo mbili nilizompelekea kwa niaba aziskize ipi angeweza kufanya vzr
ilikua hiyo ambayo mm niliita "Pendo" na "wapo"ambayo ndani alikua na
Posted by Unknown on 11:16 with No comments

Roma Mkatoliki akiongea na mabest zake Wa Mtaani huko Tanga amesema ana mpango Kuingia Kwenye Uringo wa Kisiasa ili apate nafasi Nzuri ya Kuikosoa Serikali baada ya Muziki wake Kupuuzwa na Viongozi wa Taifa hili.
“Naplan Kuzamia Kwenye Mambo ya Politics hivi sasa, By the Way Wiki Ijayo naweza Kuchukua Kadi ya Chadema Rasmi”… Pia amesema Atahakikisha Wasanii Wenzake wanaoimba Muziki wa HipHop akina Kala Jeremiah nao Wanaunda timu ya Maangamizi Kuing’oa CCM Madarakani, ila aliwasihi sana Viongozi wa Chadema Kuwa Karibu nao pale Wanapozushiwa Shutuma za ajabu ajabu Kisa Wamejiunga na Chadema.
Mpaka sasa baadhi ya wanamuziki wa Bongo Fleva waliojiunga na ambao wanampango wa kujiunga na Chama Cha kuwakomboa wanyonge CHADEMA ni Afande Sele wa Morogoro, Joseph Haule ambaye anajulikana kama Prof J, Soggy Doggy na Wengineo wengi
Subscribe to:
Posts (Atom)