Baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam kupitia hoja za mawakili wa serikali na utetezi kwenye Rufaa ya hukumu ya kifungo cha maisha jela katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’,wameamua kuhairisha rufaa hiyo mpaka tarehe husika ya kutoa hukumu ya kesi hiyo itakapopangwa hapo baadaye

Katika rufani hiyo iliyosikilizwa na jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufani ambao ni Mbarouk mbarouk, Salum Massati na Nathalia Kimaro,wakili wa upande wa mashtaka Mabele Marando amesema amekata rufaa kutokana na kutosikilizwa kwa shahidi muhimu kwenye kesi hii ambae alitajwa kuwa ndie aliwapeleka watoto hao kwa babu Seya.

Marando amesema pia ushahidi wa kuunga mkono ushahidi uliotolewa na watoto haukuzingatia sheria baada ya mahakama kutembelea nyumbani kwa babu Seya na kumuhoji mtoto bila ya kiapo hivyo ameomba Mahakama ipitie upya hukumu hiyo ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza.
Baada ya kuwasilishwa kwa maombi hayo,wakili wa serikali Jackson Bulashi akiwa na wenzake wanne amepinga maombi yaliyotolewa na upande wa mlalamikiwa na kubainisha kwamba hoja zilizowasilishwa Mahakamani zilipaswa kuwasilishwa awali wakati kesi hiyo ilipokua inasikilizwa.

Wakili huyo wa serikali ameiomba Mahakama kutupilia mbali maombi hayo kutokana na kutoainisha athari za moja kwa moja kwa washitakiwa na kutaka adhabu ya kifungo cha maisha iliyotolewa dhidi ya babu Seya na Papi Kocha iendelee kutekelezwa.
Baada ya pande zote mbili kutoa maelezo yao mbele ya jopo la majaji watatu, Mwenyekiti wa jopo hilo Jaji Nathalia Kimaro ameahirisha kesi hii ili kutoa nafasi kwa majaji kupitia maelezo yote yaliyotolewa na kuyatolea maamuzi.

Babu Seya na Papi Kocha Mwaka 2004 walihukumiwa kifungo cha maisha jela na hakimu mkazi Addy Lyamuya wa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo baada ya hukumu hiyo, February 2010 walikata rufaa Mahakama kuu ya Tanzania ambayo iligonga mwamba mbele ya jaji Thomas Mihayo wa Mahakama hiyo

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About