
Kikosi namba moja cha timu ya Mbeya City. Picha na Maktaba
IN SUMMARY
- Yanga na Simba ambazo zina rekodi nzuri ya kutwaa taji la ubingwa wa ligi zimeshindwa kutegua kitendawili hicho baada ya kulazimishwa sare na Rhino Rangers pamoja na Prisons ya Mbeya ugenini na kupoteza mchezo mmoja kila moja.
MBEYA City ambayo inasumbua vigogo kwenye Ligi Kuu Bara imezipiga bao Simba na Yanga baada ya kuzifunga timu zote zinazomilikiwa na Jeshi kwenye ligi hiyo.
Timu ya Mbeya City inayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Bara haijapoteza mchezo wowote sawa na Azam FC yenye uzoefu wa kutosha kwenye ligi hiyo.
Yanga na Simba ambazo zina rekodi nzuri ya kutwaa taji la ubingwa wa ligi zimeshindwa kutegua kitendawili hicho baada ya kulazimishwa sare na Rhino Rangers pamoja na Prisons ya Mbeya ugenini na kupoteza mchezo mmoja kila moja.
Simba ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Rhino Rangers kwenye mchezo wa kwanza sawa na Yanga iliyoshikwa na Prisons na kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na kupoteza pointi mbili kila moja.
Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imeshinda mechi sita dhidi ya timu za Jeshi na sare tano dhidi ya Yanga, Simba, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na Coastal Union.
Timu zinazomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambazo zinashiriki Ligi Kuu ni JKT Ruvu, Oljoro JKT, Ruvu Shooting, Mgambo JKT, Rhino Rangers na Prisons ya Mbeya ambayo inamilikiwa na Jeshi la Magereza.
Kwa kuzifunga timu hizo sita, Mbeya City imejikusanyia pointi 18 na kufikisha pointi 23 sawa na Azam FC ambayo ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi alisema; “Siwezi kujivuna ila nawapongeza vijana wangu kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwaomba mashabiki wazidi kutuunga mkono kwa kila hali.”
Hata hivyo, Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni aliwahi kukaririwa na Mwanaspoti akisema timu za jeshi ndizo zinazomnyima usingizi kutokana na kucheza soka la ukakamavu na bila kuchoka kwa dakika zote 90
0 comments:
Post a Comment