



Wachezaji wa Mbeya City wakipasha misuli kabla ya mtanange
Kocha huyo aliliambia Mwanaspoti kuwa hatakibadili kikosi hicho na hataafiki wachezaji kuuzwa kwani anataka kuendelea nao kwavile tayari wana msingi mzuri mpaka sasa na wameonyesha nia ya kupiga hatua.
KOCHA wa Mbeya City, Juma Mwambusi ameonya kwamba hataki kuona timu yoyote ikisogelea wachezaji wake wakati huu wa mapumziko na akasisitiza kwamba hawauzwi “Not for sale” wala hayuko tayari kufanya makubaliano yoyote.
Kocha huyo aliliambia Mwanaspoti kuwa hatakibadili kikosi hicho na hataafiki wachezaji kuuzwa kwani anataka kuendelea nao kwavile tayari wana msingi mzuri mpaka sasa na wameonyesha nia ya kupiga hatua.
“Kama ni uamuzi wangu, sitamuachia mchezaji yeyote kuchukuliwa na timu nyingine, labda uongozi kama utaamua. Nataka kuona wachezaji wangu wakiwa wale wale kwenye mzunguko wa pili kwani wamezoeana na wanajua jinsi wanavyocheza,” alisema Mwambusi akidai kwamba anatarajia baadhi ya timu zenye fedha zitaanza kuzengea wachezaji wake kama kawaida yao.
Mwambusi amekiongoza vyema kikosi cha Mbeya City kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi na haijapoteza mchezo wowote huku ikishikilia nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Azam.
Mbeya City ni kati ya timu tishio katika Ligi Kuu Bara ambayo juzi Alhamisi ilifikia tamati kwa mzunguko wa kwanza na kwa sasa timu ziko katika mapumziko hadi Januari mwakani.
0 comments:
Post a Comment