WAKATI Yanga ikicheza na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mashabiki wake walikuwa wakifanya kitu kimoja cha ajabu kidogo kwani walikuwa wakishangilia matukio yaliyokuwa yakitokea katika mchezo wa Azam FC na Mbeya City kwenye Uwanja wa Chamazi Complex.
Wakati Azam inapata bao la kwanza dakika ya 13, mashabiki wa Yanga walionekana kushangilia kwa nguvu huku wakiamini Mbeya City itasawazisha, huku wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja ya mchezo huo kupitia vituo kadhaa vya redio, mashabiki hao walilipuka kwa shangwe dakika ya 30 baada ya Mbeya City kusawazisha.


Kuna wakati mashabiki hao walikuwa wakishangilia mambo waliyokuwa wakiyasikia kutoka Chamazi Complex hali iliyokuwa ikiwachanganya wachezaji wa Yanga na Oljoro waliokuwa wakicheza kwenye Uwanja wa Taifa.
Furaha ya mashabiki hao ilirudi tena baada ya Mbeya City kupata bao la pili na hata Azam waliposawazisha ilikuwa ilikuwa vilevile. Hali hiyo kuna wakati ilikuwa ikiwasumbua mashabiki wengine ambao hawakuwa wakifuatilia mchezo huo kupitia redio ambao walikuwa wakijiuliza tukio lipi linashangiliwa Uwanja wa Taifa wakati hali inaonekana ni ya kawaida.


Huku Yanga ikiongoza kwa mabao 3-0 hadi dakika ya 85, na Azam na Mbeya City zikiwa na matokeo ya sare pia mashabiki wa Yanga walionekana wakiomba dua zote matokeo hayo yasibadilike ili timu yao ishike usukani wa Ligi Kuu ya Bara.
Hata michezo hiyo miwili ilipisha mashabiki wa Yanag kwenye Uwanja wa Taifa na wale waliokuwepo Uwanja wa Chamazi Complex, walionekana wakishangilia kwa nguvu kitu ambacho awali hawakuwa wakikifikiria sana.
Categories:

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About