Robert Lewandowski amepiga Bao 3 wakati Borussia Dortmund ilipotoka nyuma na kuibamizaStuttgart Bao 6-1 na kutua kileleni mwa Bundesliga. 
Karim Haggui aliifungia Stuttgart Bao lao mapema lakini Sokratis Papastathopoulos akasawazisha kwa kichwa na Marco Reus kufunga Bao la pili kwa Dortmund. 
Ndipo zikaja Bao 3 za Lewandowski na Pierre-Emerick Aubameyang kumalizia Bao la 6.
Tayari Msimu huu Lewandowski amepiga Bao 12 katika Mechi 14 na kuifanya Dortmund iongoze Bundesliga ikiwa Pointi 2 mbele ya Bayern Munich ambao wana Mechi moja mkononi na wanacheza Ugenini na Hoffenheim Siku ya Jumamosi.
Dortmund sasa wanaingoja Arsenal itembelee Signal Iduna Park hapo Jumatano kwa Mechi ya Marudiano ya UEFA CHAMPIONS.
 
Lewandowski akizishika nyavu za timu ya Stuttgart baada ya kuukwamisha na mpira ndani yake!
 
Kipa  Roman Weidenfeller wa Dortmund akishangilia bao la 6-1 dhidi ya Stuttgart
 
Aliyemwaga wino mpaka 2018 kocha Juergen Klopp akiwasalimia mashabiki hapo Westfalenstadion
 
Mashabiki wa Borussia Dortmund waki like na kupenda timu yao baada ya kipigo cha bao 6-1 walichokiangusha Borussia Dortimund.
 
Ushindi ni mzuri angalia staili ya kushangilia...
 
Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia baada ya kutupia bao la 6 na kufanya matokeo yabadilike na kuwa 6-1 katika dakika za lala salama dakika ya 81.
Categories:

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About