Lakini, unafahamu anachokiwaza Guardiola? Kocha huyo Mhispaniola anataka siku moja kocha wa timu pinzani atokwe na machozi ya damu. 


IN SUMMARY
  • Lakini, hilo halipo na baada ya kuwa chini ya kocha mpya, Pep Guardiola klabu ya Bayern Munich imekuwa tishio zaidi Ulaya kwa sasa pengine kuliko klabu yoyote.

MUNICH, UJERUMANI
POINTI 26 kwenye Bundesliga, tisa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ameshinda mechi nane kati ya 10 kwenye Bundesliga, huku akiwa hajapoteza yoyote na kushika usukani wa ligi hiyo ya Ujerumani.
Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ameshuka uwanjani mara tatu na kushinda zote kwenye Kundi D lenye timu pia za Manchester City, CSKA Moscow na Viktoria Plzen. Akiwa bingwa mtetezi kwenye michuano hiyo amefikisha pointi tisa, mabao 11 huku akiruhusu bao moja tu kwenye wavu wake. Eti kiwango bado.
Kwenye Bundesliga mechi 10 alizocheza na kuvuna pointi 26, amepoteza pointi nne tu baada ya kutoka sare mbili, amefunga mabao 22 na kuruhusu wavu wake uguswe mara sita. Kwa mashabiki inatosha hasa ukizingatia walitarajia timu yao ishuke kidogo kiwango kwa kuwa wachezaji wake watakuwa wamechoshwa na msimu uliopita baada ya kunyakua mataji matatu.
Lakini, hilo halipo na baada ya kuwa chini ya kocha mpya, Pep Guardiola klabu ya Bayern Munich imekuwa tishio zaidi Ulaya kwa sasa pengine kuliko klabu yoyote.
Achana na manyanyaso waliyoifanyia Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, wakati walipoinyuka timu hiyo jumla ya mabao 7-0 baada ya mechi mbili za hatua ya nusu fainali, Bayern Munich ya Guardiola, isikie hivyo hivyo.
Jose Mourinho na Chelsea yake alikiona cha moto kwenye Super Cup licha ya kiburi chake, kabla ya Manchester City kukumbana na dhahama kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya tena wakiwa nyumbani Etihad. Bayern Munich ni hatari sana.
Lakini, unafahamu anachokiwaza Guardiola? Kocha huyo Mhispaniola anataka siku moja kocha wa timu pinzani atokwe na machozi ya damu.
Ligi ya Mabingwa Ulaya
Bayern Munich mechi yao iliyopita walimkung’uta Viktoria Plzen mabao 5-0 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ilimiliki mchezo huo kwa asilimia 77 kwa maana Plzen walikuwa wanakimbiza vivuli vya wenzao tu ndani ya uwanja.
Walipiga mashuti 18 yaliyolenga lango la Plzen, wakati wapinzani hao hawakupiga hata shuti moja na hakuwa mchezaji yeyote wa Bayern Munich aliyeonyeshwa hata kadi ya njano.
Mabingwa hao wa mataji matatu msimu uliopita, hawajapoteza mechi yoyote msimu huu tangu walipofungwa na Borussia Dortmund kwenye DFB Super Cup

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About