Kocha wa Arsenal Arsene Wenger vita yake ya kesho ili kushinda mechi hiyo anataka wachezaji matata wa Liverpool Sturdge na Luis Suarez kukabwa vilivyo na wachezaji wake ili wasiweze kuliona lango lao. Mzee huyo wa Gunners pamoja na kumuona Suarez ni mwingi wa tabia mbaya lakini bado anamuhitaji klabuni kwake na japo alimkosa msimu huu wa 2013/14.  Kocha huyo pia anamwamini Mesut Ozil pamoja na Santi Carzorla na anaamini kuwa wako fiti kwa mchezo wa kesho na anasema wataleta mabadiliko kwenye mtanange huo ambao wao Arsenal wapo kileleni kwa pointi 22 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Chelsea wakiwa na alama 20 wakifuatiwa na Liverpool ambao wana alama pia 20 sawa na Chelsea hivyo kama watawafunga Liverpool wataendelea kushikilia nafasi hiyo ya kuongoza na kama watakosa nafasi hiyo nafasi hiyo itashikiliwa na Chelsea au Liverpool itategemea nani atakwama na nani anafunga.
All smiles: Mesut Ozil (left) and Santi Cazorla (right) are fit for Saturday's top-of-the-table clash 
Kwenye mazoezi Mesut Ozil na  Santi Cazorlawakifurahia jambo huku wakiwa na furaha kwa timu yao kuwa juu kileleni.
Kocha Arsene Wenger yupo juu kileleni kwa sasa lakini nyuma yake nafasi ya tatu kuna mzee Rogers anayekinoa kikosi cha Liverpool kinachofanya vyema kwa sasa kutokana na ushirikiano safi wa wafungaji wake Suarez na Sturridge. Kesho mtanange huo unakitendawili cha aina yake, dakika 90 ni jibu tosha! 
Majembe mawili hatari: Luis Suarez na Daniel Sturridge tarajiwa kuwepo kesho jumamosi kwenye patashika na wote wawili wana kutafuta ushindi kwa timu yao.Historia ya Liverpool katika mitanange iliyopita
 
Arsene Wenger baada ya kufungwa na kutupwa nje kwenye Capital One Cup na Chelsea nyumbani Emirates kesho anataka kufuta upuuzi huo wa kufungwa tena mfululizo klabuni hapo Emirates.
 
Wenger pia anaamini kuwa majembe Sturridge na Suarez ni moja ya wafungaji hatari kwenye ligi hiyo pendwa Duniani na kesho Jumamosi kunachangamoto zake. Hivyo amewaeleza wachezaji wake kuwa makini zaidi na watu hao na kuweka umakini sana ili washinde waendelee kuongoza msimu huo.
 
Mesut Ozil ni moja ya wachezaji wa kwanza wa Arsenal wa kikosi cha kwanza dhidi ya Liverpool kesho. 
Kwenye Mazoezi wachezaji wa Liverpool wakipewa somo na kocha wao Brendan Rodgers akiwa na kijana machachali Philippe Coutinho kwa karibu ambapo pia wenda kesho akacheza dhidi ya Gunners.
 
Mchezaji Mathieu Flamini yeye atakuwa nje wakati wa mtanange na Liverpool baada ya kupata majeraha hivi karibuni wiki iliyopita wakati wanacheza naCrystal Palace.



Refa wa kila mtanange kesho Jumamosi Raundi ya 10
DATEK.O.MATCHESSTADIUMREFEREE
Sat 2 Nov 201312:45Newcastle v ChelseaSt James' ParkLee Mason
Sat 2 Nov 201315:00Fulham v Man UtdCraven CottageLee Probert
Sat 2 Nov 201315:00Hull v SunderlandThe KC StadiumAndre Marriner
Sat 2 Nov 201315:00Man City v NorwichEtihad StadiumPhil Dowd
Sat 2 Nov 201315:00Stoke v SouthamptonBritannia StadiumChris Foy
Sat 2 Nov 201315:00West Brom v Crystal PalaceThe HawthornsNeil Swarbrick
Sat 2 Nov 201315:00West Ham v Aston VillaBoleyn GroundHoward Webb
Sat 2 Nov 201317:30Arsenal v LiverpoolEmirates StadiumMartin Atkinson
Sun 3 Nov 201313:30Everton v SpursGoodison ParkKevin Friend
Sun 3 Nov 201316:00Cardiff v SwanseaCardiff City StadiumMike Dean



RATIBA KESHO JUMAMOSI.
Jumamosi 2 Novemba
15:45 Newcastle United v Chelsea
18:00 Fulham v Manchester United
18:00 Hull City v Sunderland
18:00 Manchester City v Norwich City
18:00 Stoke City v Southampton
18:00 West Bromwich Albion v Crystal Palace
18:00 West Ham United v Aston Villa
20:30 Arsenal v Liverpool
Jumapili 3 Novemba
19:30 Everton v Tottenham Hotspur
22:00 Cardiff City v Swansea City
Categories:

0 comments:

Post a Comment

    Blogger news

    Blogroll

    Pages

    About